Papa Leo XIV,amani kwa ajili ya Ira,Syria&Ukraine:mazungumzo na uvumilivu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, akiwageukia waamini na mahujaji waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, Dominika tarehe 11 Januari 2026 ikiwa ni Sherehe za Ubatizo wa Bwana Wetu Yesu, Baba Mtakatifu alisema: “Kaka na dada wapendwa, kama nilivyokwisha sema, asubuhi ya leo, kulingana na desturi ya Siku kuu ya Ubatizo wa Yesu, niliwabatiza watoto wachanga kadhaa, watoto wa wafanyakazi wa Makao Matakatifu.”
Baraka kwa watoto wote
Papa Leo kuhusu watoto aliendelea kusema: “Na sasa ningependa kuwapatia baraka zangu watoto wote waliopokea au watakaopokea Ubatizo katika siku hizi, huku Roma na ulimwenguni kote, nikiwakabidhi kwa ulinzi wa Mama wa Bikira Maria.” Papa Leo aliendelea kusema “Ninawaombea hasa watoto waliozaliwa katika hali ngumu zaidi, katika afya na kutokana na hatari za nje. Neema ya Ubatizo, inayowaunganisha na Fumbo la Pasaka la Kristo, ifanye kazi kwa ufanisi ndani yao na katika familia zao.”
Mawazo kwa Mashariki ya Kati: Iran ina Syria
Papa Leo XIV aidha alielekea nchi ambazo zimegubikwa ma vurugu na kusema: “Mawazo yangu yanageukia kile kinachotokea siku hizi Mashariki ya Kati, hasa Iran na Syria, ambapo mvutano unaoendelea unasababisha vifo vya watu wengi. Natumaini na kuomba kwamba mazungumzo na amani vitaendelezwa kwa uvumilivu, ili kutafuta manufaa ya jamii kwa ujumla.” Papa alikumbusha Nchi ya Ulaya Mashariki kwamba, “Nchini Ukraine, mashambulizi mapya, hasa makubwa, yanayolenga miundombinu ya nishati, yanaathiri vibaya raia, huku hali ya hewa ya baridi ikizidi kuwa mbaya. Ninawaombea wale wanaoteseka na kufufua wito wangu wa kukomesha vurugu na kuimarishwa kwa juhudi za kufikia amani.”
Salamu kwa mahujaji
“Na sasa ninawasalimu wote, Warumi na mahujaji mliopo leo katika Uwanja wa Mtakatifu Petro,” kwa njia hiyo Papa aliongoza kusema kwa lugha ya kiingereza na kihispania (thank you, muchas gracias!)”asanteni, shukrani nyingi! Kwa namna ya pekee, ninawasalimu kikundi kutoka Shule ya "Everest" ya Madrid na chama cha "Bambini Fratelli" cha Guadalajara, Mexico: Dejemos que los niños sueñen” yaani "Tuwaache watoto waote ndoto."Ninawatakia nyote Dominika njema!
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.