Papa alitua katika Las Palmas de Gran Canaria!
Vatican News
Baba Mtakatifu Leo XIV alitua katika kituo cha anga cha Gran Canaria-Gando, saa 4.38 asubuhi siku ya Alhamisi, tarehe 11 Juni 2026, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kitume katika visiwa vikubwa vya Bahari ya Atlantiki, pia vitajumuisha kituo huko Santa Cruz de Tenerife, Papa atahitimisha ziara yake ya nne ya kitume nchini Hispania tarehe 12 Juni 2026.
Baba Mtakatifu Leo XIV aliondoka kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Josep Tarradellas Barcelona-El Prat kuelekea Las Palmas de Gran Canaria saa 2.45, Alhamisi asubuhi tarehe 11 Juni 2026. Hii inakuwa kituo cha tatu cha Ziara yake ya kitume, mara baada ya kuadhimisha misa katika Basilika ya Familia Takatifu huko Barcelona usiku wa tarehe 10 Juni 2026 na kuzindua mnara wa Kanisa Kuu hilo.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here
