2026.06.11  Papa amewasili katika  Gran Canaria-Gando. 2026.06.11 Papa amewasili katika Gran Canaria-Gando.  (@Vatican Media)

Papa alitua katika Las Palmas de Gran Canaria!

Baba Mtakatifu akihitimisha na Ibada ya Misa Takatifu tarehe Juni 10,katika Kanisa Kuu la Sagrada Familia,ilikuwa ni mwisho wa awamu ya ziara yake ya kitume huko Barcelona na kufungua hatua nyingine kwa kutua katika visiwa vikubwa vya Bahari ya Atlantiki.Tukio la kwanza litakuwa mkutano na vituo vya mapokezi ya wahamiaji tarehe 11 Juni 2026 na kufuatiwa Mkutano wa Kanisa na Misa.

Vatican News

Baba Mtakatifu Leo XIV alitua katika kituo cha anga cha Gran Canaria-Gando,  saa 4.38  asubuhi siku ya Alhamisi, tarehe 11 Juni 2026, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kitume katika visiwa vikubwa vya Bahari ya Atlantiki, pia vitajumuisha kituo huko Santa Cruz de Tenerife, Papa atahitimisha ziara yake ya nne ya kitume nchini Hispania tarehe 12 Juni 2026.

Baba Mtakatifu Leo XIV aliondoka kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Josep Tarradellas Barcelona-El Prat kuelekea Las Palmas de Gran Canaria saa 2.45, Alhamisi asubuhi  tarehe 11 Juni 2026. Hii inakuwa kituo cha tatu cha Ziara yake ya kitume, mara baada ya kuadhimisha misa katika Basilika ya Familia Takatifu huko Barcelona usiku wa tarehe 10 Juni 2026 na kuzindua mnara wa Kanisa Kuu hilo.


Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

11 Juni 2026, 12:19