Tafuta

2026.07.24: Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Baraza la Maaskofu Asia(FABC). 2026.07.24: Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Baraza la Maaskofu Asia(FABC). 

Kard.Grech:Kanisa la Asia katika kipaumbele cha Safari ya Sinodi

Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu katika Mkutano Mkuu wa XII wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Asia(FABC),unaoendelea Jakarta,Indonesia,hadi Dominika Julai 26 alitoa hutuba yake iliyojikita na mada:“ Uongofu wa Sinodi na Utume wa kuwa Madaraja na Wajenzi wa Madaraja Asia.” Kardinali alitoa mwaliko wa thamani ya upamoja kati ya Makanisa,yanayoitwa kushirikishana uzoefu na zawadi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu, Kardinali Mario Grech alitoa hotuba yake tarehe 24 Julai 2026  kwa Mkutano Mkuu wa XII wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Asia(Fabc) waliounganika huko Jakarta nchini Indonesia utakaohitimishwa Dominika tarehe 26 Julai 2026. Katika Kanisa la Asia katika kwenye safari ya kisinodi, haimanishi kuzungumza kisinodi tu, bali kutafuta namna ya kuishi katika maisha ya kawaida ya Makanisa yetu.” Kwa maneno, Kardinali  Grech, hotuba ilikuwa na mada, ta matazamio msingi wa “hatua inayofuata ya Sinodi kuhusu hali ya Kisinodi: kipaumbele cha Makanisa mahalia.” Suala la hatua ya kwanza ya sasa na katika safari ya Mkutano, awali ya yote ni Kanisa mahalia ambalo halina thamani ya "kiupangaji tu.

Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Asia
Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Asia   (web)

Kanisa mahalia kwa hakika pamoja na kuwa limegawanyika kiutawala wa Kanisa la Ulimwengu tu, ni  onesho la kweli la Kanisa mahalia, ambapo Injili ni tangazo, sakramenti zinaadhimishwa na waamini wanaungna katika umoja na Kristo.” Katika hotuba yake kwenye Mkutano huo kwa mada “Mwaliko wa uongofu wa kisinodi na utume wa kuwa madaraja na wajenzi wa madaraja barani Asia,” Katibu Mkuu wa Sinodi alikumbusha kuwa, Kanisa la ulimwengu wote haliwezi kuchukuliwa kama ukweli wa kufikirika uliojitenga na jumuiya halisi ambazo linaishi. “Ikiwa Kanisa mahalia halitoi mchango wake binafsi, linakosesha Kanisa mahalia chochote cha kuishi,” kwa sababu “kila Kanisa mahalia linachukua zawadi, uzoefu, rasilimali na ishuhuda wa kipekee.”

Kwa kupitia safari ya kisinodi iliyoanzishwa kunako 2021, Kardinali aliuliza swali ambalo liliongoza mchakato: Ni kwa jinsi gani ya kifikia watu wa Mungu? Kutoka katika mtazamo huo ndilo inatokea chaguo stahiki: “Ushiriki wa wote hauwezi kuwa maudhui tu, bali zaidi ya yote mbinu.” Na wakati huo huo, Watu wa Mungu wasingeweza kuwa wahusika kwa urahisi tu, badala yake  walipaswa  hasa kuwa wahusika katika safari.” Kwa sababu hiyo “kusikiliza Kanisa na hii ilikuwa  msingi, kwa sababu Kanisa la Kisinodi ni Kanisa la kusikiliza, maana, udhabiti, na kusikiliza makanisa.”


Thamani ya ushirikiano kati ya makanisa

Kardinali Grech alitoa mwaliko wa thamani ya upamoja kati ya Makanisa, yanayoitwa kushirikishana uzoefu na zawadi. Mchakato wa kisinodi, hautazamii tu uzalishaji wa maandishi mapya tu, bali kusaidia mzunguko wa zawadi ambao unaongeza nguvu ya umoja na kusaidia utume.” Moja ya mapya yaliyojitokeza katika safari ya kisinodi ilikuwa ni  hatua ya mchakato ambao ulirudi katika jumuiya mahalia ili kukaribishwa kwa upya. “Harakati kwa hivyo haikuwa ya upande mmoja tu, bali ya pande mbili, na kiukweli ilikuwa ya mzunguko,” alisisitiza Kardinali Grech.

Kazi ya Sinodi isitenganishwe na maisha ya kweli ya Jumuiya

Ni chaguo  la lazima, kwa sababu kazi ya kisinodi isitenganishwe na maisha ya kweli ya jumuiya: ni kwa kusiliza tu na kusikiliza tena Makanisa mahalia, yaani Watu wa Mungu katika mwili na mfupa, unaundwa na wanaume na wanawake waliobatizwa, kwamba inawezakana kuwa na uhakika kuwa kazi ya idadi ndogo ya wataalam, ambayo haiishi tu kuwa ya kupitia juu kwa misingi ya kikanisa.”

Maaskofu wa Bara la Asia
Maaskofu wa Bara la Asia

Sinodi siyo hati au maamuzi rahisi, ni uzoefu wa kuishi katika makanisa

Kwa kuwaelekea kwa namna ya pekee Kanisa barani Asia, alisisitiza uzito wa uzoefu wake: mazungumzo na dini, wingi wa tamaduni, hali ambayo mara kadhaa wanaipata wakristo wachache na ukaribu wa maskini, unawakilisha maeneno ambayo roho inaendelea kutenda.“Swali msingi awali ya yote si jinsi gani Makanisa ya Asia yatapokea nini kutoka katika Sinodi, badala yake, ni zawadi gani ya Roho Mtakatifu wanaitamani itolewe kwa njia yake na kwa Kanisa zima.”

Kanisa linaendelea kukua kama ushirika na kama utume

Hatua ya sasa, inayoendelea kupokea, itakuwa maamuzi kwa kile ambacho kuna mantiki nyingi, hasa muhimu zaidi, ambapo Kardinali Grech alitangaza, akikumbusha kuwa, Sinodi haiwezi kubaki katika hati, au maamuzi rahisi, lakini linapaswa kugeuka kuwa uzoefu unaoushi katika Makanisa. Hata nafasi ya Maaskofu, imeakisiwa na matarajio ya Sinodi. Sinodi siyo masuala ya ushiriki tu,   bali ni fursa kwa ajili ya kutambua zaidi huduma ya kina ya mamlaka yaliyokabidhiwa Askofu wa Jimbo.” Askofu anaitwa kusikiliza watu wa Mungu na kuwasindikia katika changuzi za kikanisa, kwa kulinda umoja.” Hali ya sasa ya Sinodi itapelekea tunda lake zaidi ikiwa kila Kanisa mahalia litajitambua lenyewe na wakati huo, kama mwelekeo na kama mbebaji wa zawaidi,” na kuhitimisha akisema kwamba katika tunda hili kuna mabadilishano kati ya Kanisa, “ Kanisa linaendelea kukua  kama ushirika na kama utume.”

HOTUBA YA KARD GRECH

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

24 Julai 2026, 15:43