Tafuta

2026.07.21 XII Picha ya Pamoja na Maaskofu wa Shirikisho la mabaraza ya Maaskofu wa Asia (FABC) 2026.07.21 XII Picha ya Pamoja na Maaskofu wa Shirikisho la mabaraza ya Maaskofu wa Asia (FABC)  

Kard.Tagle kwa Fabc:Mtazame Kristo,Mjenzi wa Daraja la Kweli!

Katika Mkutano Mkuu wa 12 wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Asia(FABC),unaoendelea Jakarta,Indonesia,Julai 22 ilikuwa Siku ya Maombi na Mafungo ya Kiroho. Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji:Kabla ya "kuunda mikakati,lazima turudi kumtazama Yesu,kumtafakari na kujifunza kutoka Kwake.Kanisa halipaswi kuwa juu ya watu wa Mungu:wachungaji wameitwa kuwatumikia waamini."

Vatican News

Wakristo wanaweza kuwa wajenzi wa madaraja kwa kukutana na Kristo kwa mara ya kwanza, daraja la kweli kati ya mbingu na dunia, Yule ambaye kupitia yeye Mungu, ubinadamu, na viumbe vyote "vinashikamana." Hili lilisisitizwa Jumatano tarehe 22 Julai 2026 na Kardinali Luis Antonio Tagle, Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji - Sehemu ya Uinjilishaji wa Kwanza na Makanisa Mapya Maalum, akizungumza katika Mkutano Mkuu wa 12 wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Asia (FABC). Mkutano huo, unaoendelea hadi Dominika tarehe 26 Julai  huko Jakarta, Indonesia, kwa kuongozwa mada: "Wito wa Uongofu wa Sinodi na Utume wa kuwa Madaraja na Wajenzi wa Madaraja Asia."

Usikae mbali na ubinadamu na uumbaji

Kardinali Tagle ambaye mnamo 2007 alikuwa rais wa Ofisi ya Masuala ya Taalimungu ya FABC aliongoza Siku ya Maombi na Mafungo ya Kiroho huku akizingatia tafakari yake juu ya kifungu cha Injili kutoka Injili ya  Yohane ambapo Yesu anamwambia Nathanaeli: "Mtaona mbingu zimefunguliwa, na malaika wa Mungu wakipanda na kushuka juu ya Mwana wa Adamu" (1:43-51). Kwa hivyo, alisisitiza ukweli kwamba Kristo anaunganisha uhusiano wa wima kati ya Mungu na ubinadamu na uhusiano wa usawa kati ya watu na uumbaji. Kwa hivyo, Kardinali alisema, "kuwa na Mungu haimaanishi kuwa mbali na ubinadamu na uumbaji."

Il cardinale Luis Antonio Tagle, Pro-Prefetto del Dicastero per l'Evangelizzazione - Sezione per la prima evangelizzazione e le nuove Chiese

Kardinali Luis Antonio Tagle,Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji (@ FABC 12 Assembly 2026)

Wito wa kuwa na Roho ya Huduma

Wakati huo huo, Kardinali Tagle alionya dhidi ya mitazamo ambayo inaweza kuwaweka wachungaji wa Kanisa juu sana, na mbali sana na watu wa Mungu ambao wameitwa kuwatumikia. Alielezea kwamba kuja kwa Yesu duniani hakukuwa kitendo cha kujishusha, bali badala yake ilikuwa upendo kwa  walio wake mwenyewe."

Umuhimu wa kukutana kuliko mikakati

Kardinali Tagle pia alihimiza sana "kurudi kumtazama Yesu, kumgusa, kumwona, kumtafakari, na kujifunza kutoka kwake," akipaupatia kipaumbele kukutana na Kristo kuliko "kuendeleza mikakati." Huu ni mwaliko muhimu katika bara lililojaa changamoto za changamano za kijamii.

Mbinu ya "mazungumzo katika Roho"

Siku hiyo iliadhimishwa na maombi ya kimya kimya, kutafakari, na "Mazungumzo katika Roho," njia ya utambuzi ambayo imekuwa alama ya safari ya sinodi ya Kanisa. Katika suala hili, Tagle alihitimisha kwa kuwatia moyo waliohudhuria kusali kwa picha za kibiblia na si dhana za kufikirika, kwa sababu alama kama vile madaraja, ngazi, na mbingu zilizo wazi zinaweza kufichua vipimo vya ndani zaidi vya fumbo la Mungu.

Kardinali Gracias:kujenga amani na udugu barani Asia

Kardinali Oswald Gracias, Askofu Mkuu Mstaafu wa Bombay na Mjumbe Maalum wa Papa katika mkutano mkuu, badala yake alilenga utume wa Kanisa kama chombo cha amani na upatanisho. Akiongoza sherehe ya kwanza ya Misa takatifu Jumanne tarehe 21 Julai 2026, Kardinali wa India ambaye aliwahi pia kuwa rais wa zamani wa Shirikishio hilo la FABC kuanzia 2011 hadi 2018, alitaja changamoto kadhaa za enzi ya kisasa, ikiwa ni pamoja na vita na vurugu. Alisema, kwa kukabiliana na haya, Kanisa la Asia linaitwa kupyaisha ahadi yake ya kutangaza Injili. Akiwatia moyo waliohudhuria "kutafuta njia mpya na za ubunifu za kujenga amani na udugu barani," Kardinali Gracias alihitimisha kwa kugusia sinodi, akiiita  kama "zawadi"kwa Kanisa na Jumuiya ya  Asia, kwani inahusisha kusikiliza, kushiriki, uwazi, na uwajibikaji wa pamoja.

Il cardinale Oswald Gracias, arcivescovo emerito di Bombay e Inviato Speciale del Papa

Kardinali  Oswald Gracias, Askofu Mkuu Mstaafu wa Bombay na Mjumbe Maalumu wa Papa(@ FABC 12 Assembly 2026)

Umoja wa Kanisa katika Utofauti wa Watu na Tamaduni

Makardinali na maaskofu  zaidi ya mia moja, mapadre, watawa, na wajumbe kutoka barani kote Asia  walisherehekea pamoja na Mjumbe Maalum wa Papa. Misa  iliadhimishwa na Makardinali Stephen Sau-yan Chow, SJ, Askofu wa Hong Kong, na Virgilio do Carmo da Silva, SJ, Askofu Mkuu wa Dili, Timor- ya Mashariki. Katika Sala ya Waamini,  nia zilitolewa katika lugha kadhaa za Asia, zikisisitiza umoja wa Kanisa miongoni mwa watu, tamaduni, na lugha nyingi za bara hilo.

Askofu Subianto:kusikiliza,kushirikishana na maono ya pamoja 

Wakati huo baada ya Misa,  Askofu Antonius Franciskus Subianto Bunjamin, wa Jimbo katoliki la Bandung na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Indonesia, alifungua shughuli za Mkutano wa 12 wa FABC, huku akisisitiza kwamba tukio hilo linawakilisha "zaidi ya mkutano rahisi na Maaskofu: ni wakati mtakatifu wa kumsikiliza Roho Mtakatifu, kusikilizana, na kusikia sauti za watu wa Asia."

Monsignor Antonius Franciskus Subianto Bunjamin, vescovo di Bandung e presidente della Conferenza episcopale cattolica indonesiana

Askofu Antonius Franciskus Subianto Bunjamin,wa Bandung na Rais wa Baraza la Maaskfofu Katoliki wa indonesiana(@ FABC 12 Assembly 2026)

Mihimili minne ya mazungumzo

 Askofu wa Shirika la Msalaba Mtakatifu, aliongeza kuwa mazungumzo ni sifa tofauti ya Kanisa la Asia na yamepangwa kwa misingi mitatu: mazungumzo na maskini, na tamaduni, na dini zingine. Kwa haya, Askofu wa Indonesia alibainisha, nyingine sasa imeongezwa ya : mazungumzo na Nyumba yetu ya  Pamoja, ambayo imekuwa kipimo muhimu zaidi cha utume wa Kanisa akiwa na maana ya utunzaji wa mazingira. Askofu wa Subianto kisha aliwahimiza washiriki kuimarisha uongofu wao wa sinodi kupitia kusikiliza, kushirikiana, na maono ya pamoja kwa ajili ya siku zijazo, akihitimisha kwa kukumbusha mwaliko wa Papa Leo XIV kwa Kanisa linalojenga madaraja kupitia upendo.

Ikumbukwe katika Barua yake kwa Kardinali Gracias, mjumbe wake maalum kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa XII wa Shirikisho la Mabaraza  ya Maaskofu wa Asia (FABC), uliofunguliwa huko  Jakarta, Indonesia, kuanzia tarehe 20 hadi 26 Julai 2026, Papa Leo XIV alikuwa amewaalika waamini na Maaskofu, kama ilivyo katika waraka wa "Magnifica Humanitas", kumweka Mungu " kwenye upeo wa matendo yetu na mwanadamu katikati ya chaguo zetu", bila hofu ya "kuchafua mikono yetu katika eneo la ujenzi la wakati wetu." Aidha Baba Mtakatifu alikuwa amewambia " kila mtu kusimamisha ujenzi wa Babeli nyingine na kuunganisha nguvu ili kujenga katika wema, ili ubinadamu usipoteze uzuri wake na ulimwengu uweze kutambua tena, katika moyo wa mwanadamu, mahali ambapo Mungu anataka kukaa."

MKUTANO MKUU WA 12 WA MAASKOFU ASIA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

22 Julai 2026, 20:29