Jukwaa la PATH:Taalimungu lazima iunganishe taaluma kwa umakini wa kisayansi
Na Padre Paweł Rytel-Andrianik – Vatican.
Wakati akihitimisha mkutano wa Kimataifa uliofanyika mjini Roma kuanzia tarehe 6 na 7 Machi 2026, akinukuu Barua Binafsi ya Motu Proprio ya Papa Francisko (1Novemba 2023) ya “Ad Theologiam Promovendam,” inayojikita inahusu idhini ya Katiba mpya za Vyuo Vikuu vya Kipapa vya Taalimungu), Askofu Antonio Stagliano, Rais wa Chuo cha Kipapa cha Taalimungu (PATH), alianisha kanuni kuu tatu elekezi kwa taalimungu ya sasa.
Umoja, Hekima na Mshikamano
Kwa kuanzia, Askofu Staglianò alisisitiza umuhimu wa kukuza umoja wa vipengele vya Taalimungu ya kisayansi, kihekima (satiential) na kimshikamano. “Vitu hivi siyo chaguo mbadala, bali ni vipengele msingi vinavyounda wito mmoja,” alibainisha. Taalimungu inayojikita kwenye sayansi tu inaweza kuwa hatarishi na kuwa maarifa makavu yasiyo na matunda. Wakati huo huo, taalimungu inayokazia hekima pekee inaweza kuangukia katika hisia za kupita kiasi (sentimentalism), wakati taalimungu inayojikita katika mshikamano tu inaweza kupoteza misingi wake wa ukweli. Askofu huyo alibanisha kuwa, chagamoto ni kuunganisha vipengele hivi katika utafiti, ufundishaji na maisha.
Wakati wa mkutano wa Chuo cha Kipapa cha Taalimungu, mjini Roma.
Ujasiri na Unyenyekevu katika Mazungumzo
Pili, Askofu Staglianò aliwasihi Wataalimungu kuendeleza mazungumzo ya kuvuka taaluma mbalimbali kwa ujasiri na unyenyekevu. Kukubali kutoka nje ya maeneo ya tunayoyapenda, na kushiriki katika mijadala yenye lugha za kielimu zisizoelezeka ni jambo la muhimu. Vivyo hivyo, unyenyekevu utuongoze kubainisha kuwa Taalimungu haina majibu ya maswali yote, japo inaweza kuibua maswali msingi, juu ya maana, utu na hatima ya ubinadamu na ulimwengu.
Taalimungu kama huduma katika Kanisa na Ulimwengu
Askofu huyo aidha aliwakumbusha washiriki kuwa, Taalimungu ni kwa ajili ya huduma kwa Kanisa, na kwa Ulimwengu. Akirejea mkutano wa Papa Leo XIV na wanataaluma, hao alisisitiza kwamba Wataalimungu wameitwa kuwasilisha “maarifa” pamoja na “utamu” wa imani, ili iweze kuangaza maisha ya watu na kukuza ulimwengu wa kidugu na mshikamano duniani.
Kujenga Mtandao wa Kimataifa wa Taalimungu ya Kihekima
Jukwaa hilo aidha liliwasilisha pia mipango ya baadaye ya PATH, ikiwemo kuanzishwa kwa Mtandao wa kimataifa wa Taalimungu ya Hekima (Sapiential theology),mfumo wa pamoja wa kimuundo kwa wawakilishi wa kanda mbalimbali, na Mkutano ya Kitaalimungu, ya mada maalum inayoshughulikia masuala makubwa ya nyakati za sasa. Akitoa muhtasari wa majadiliano hayo, Askofu Staglianò alihitimisha kuwa kulijitokeza imani ya pamoja kutoka katika jukwaa hilo: “Taalimungu ya siku zijazo itakuwa ya kuvuka mipaka ya taaluma mbalimbali au haitakuwepo kabisa.”
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.