Askofu Antonio Staglianò, Rais wa Chuo cha Kipapa cha Taalimungu. Askofu Antonio Staglianò, Rais wa Chuo cha Kipapa cha Taalimungu. 

Jukwaa la PATH:Taalimungu lazima iunganishe taaluma kwa umakini wa kisayansi

Katika jukwaa la PATH lililofanyika mjini Roma,Machi 6-7,Askofu Antonio Stagliano,Rais wa Chuo cha Kipapa cha Taalimungu(PATH)alisisitiza kwamba,"mustakabali wa Taalimungu unapaswa kuvuka mipaka ya taaluma mbalimbali,ukiunganisha umakini wa kisayansi,hekima ya hali ya juu na mshikamano na daima kutumikia Kanisa na Ulimwengu."

Na Padre Paweł Rytel-Andrianik – Vatican.

Wakati akihitimisha mkutano wa Kimataifa uliofanyika mjini Roma kuanzia tarehe 6 na 7 Machi 2026, akinukuu  Barua Binafsi ya Motu Proprio ya Papa Francisko (1Novemba 2023) ya “Ad Theologiam Promovendam,” inayojikita inahusu idhini ya Katiba mpya za Vyuo Vikuu vya Kipapa vya Taalimungu), Askofu Antonio Stagliano, Rais wa Chuo cha Kipapa cha Taalimungu (PATH), alianisha kanuni kuu tatu elekezi kwa taalimungu ya sasa.

Umoja, Hekima na Mshikamano

Kwa kuanzia, Askofu Staglianò alisisitiza umuhimu wa kukuza umoja wa vipengele vya Taalimungu  ya kisayansi, kihekima (satiential) na kimshikamano. “Vitu hivi siyo chaguo mbadala, bali ni vipengele msingi vinavyounda wito mmoja,” alibainisha. Taalimungu inayojikita  kwenye sayansi tu inaweza kuwa hatarishi na kuwa maarifa makavu yasiyo na matunda. Wakati huo huo, taalimungu inayokazia hekima pekee inaweza kuangukia katika hisia za kupita kiasi (sentimentalism), wakati taalimungu inayojikita katika mshikamano tu inaweza kupoteza misingi wake wa ukweli. Askofu huyo alibanisha kuwa, chagamoto ni kuunganisha vipengele hivi katika utafiti, ufundishaji na maisha.

Forum of the Pontifical Academy of Theology

Wakati wa mkutano wa  Chuo cha Kipapa cha Taalimungu, mjini Roma.

Ujasiri na Unyenyekevu katika Mazungumzo

Pili, Askofu Staglianò aliwasihi Wataalimungu  kuendeleza mazungumzo ya kuvuka taaluma mbalimbali kwa ujasiri na unyenyekevu. Kukubali kutoka nje ya maeneo ya tunayoyapenda, na kushiriki katika mijadala yenye lugha za kielimu zisizoelezeka ni jambo la muhimu. Vivyo hivyo, unyenyekevu utuongoze kubainisha kuwa Taalimungu haina majibu ya maswali yote, japo inaweza kuibua maswali msingi, juu ya maana, utu na hatima ya ubinadamu na ulimwengu.

Taalimungu kama huduma katika Kanisa na Ulimwengu

Askofu huyo aidha aliwakumbusha washiriki kuwa, Taalimungu ni kwa ajili ya huduma kwa Kanisa, na kwa Ulimwengu. Akirejea mkutano wa Papa Leo XIV  na wanataaluma, hao  alisisitiza kwamba Wataalimungu  wameitwa kuwasilisha “maarifa” pamoja na “utamu” wa imani, ili iweze kuangaza maisha ya watu na kukuza ulimwengu wa kidugu na mshikamano duniani.

Kujenga Mtandao wa Kimataifa wa Taalimungu ya Kihekima

Jukwaa hilo aidha  liliwasilisha pia mipango ya baadaye ya PATH, ikiwemo kuanzishwa kwa Mtandao wa kimataifa wa Taalimungu ya Hekima (Sapiential theology),mfumo wa pamoja wa kimuundo kwa wawakilishi wa kanda mbalimbali, na Mkutano ya Kitaalimungu, ya mada maalum inayoshughulikia masuala makubwa ya nyakati za sasa. Akitoa muhtasari wa majadiliano hayo, Askofu  Staglianò alihitimisha kuwa kulijitokeza imani ya pamoja kutoka katika jukwaa hilo: “Taalimungu ya siku zijazo itakuwa ya kuvuka mipaka ya taaluma mbalimbali au haitakuwepo kabisa.”

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

11 Machi 2026, 17:09