Tafuta

2018.12.17 Pena di Morte, esecuzione capitale, death penalty

Cuba yawaachilia wafungwa 51 wakati wa Juma Takatifu kufuatia mazungumzo na Vatican

Katika taarifa ilitolewa na serikali ya Cuba,ilisema uamuzi wa kuwasamehe wafungwa kadhaa katika siku zijazo uliochukuliwa kwa moyo wa nia njema na uhusiano wa kidiplomasia unaobadilika na Vatican na unaendana na ukaribu wa Maadhimisho ya Juma Takatifu.

Vatican News

Akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari,  msemaji Mkuu wa Ofisi ya  vyombo vya Habari vya Vatican Bwana  Matteo Bruni alithibitisha tarehe 13 Machi 2026 kwamba kumekuwa na majadiliano ya hivi karibuni kati ya Vatican  na mamlaka ya Cuba "kuhusu kuachiliwa kwa wafungwa" katika Serikali ya  kisiwa cha Carribean. Hii inafuatia taarifa iliyotolewa  tarehe 12 Machi 2026  na maafisa wa Cuba iliyosema, "Katika moyo wa nia njema na uhusiano wa karibu na unaobadilika kati ya Serikali ya Cuba na Vatican, uhusiano ambao mawasiliano yamedumishwa kihistoria,  kuhusu michakato ya mapitio na kuachiliwa kwa watu walionyimwa uhuru, Serikali ya Cuba imeamua kuwaachilia, katika siku zijazo, watu 51 walio gerezani." Taarifa hiyo pia inabainisha kuwa, wote ni wafungwa ambao wamedumisha tabia njema wakiwa gerezani kwa sehemu kubwa ya kifungo chao.

Tendo la  Cuba

Serikali iliendelea kuelezea kwamba zaidi ya wafungwa 9,900 wamefaidika na msamaha tangu 2010. Iliongeza kusema kwamba "zaidi ya hayo, katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kama sehemu ya tendo la Cuba na kwa mujibu wa vifungu vya sheria, watu wengine 10,000 wanaotumikia vifungo vya gerezani wameachiliwa huru kupitia aina mbalimbali za  manufaa ya kisheria."

Juma Takatifu

Hatimaye, taarifa hiyo inaelezea kwamba uamuzi huo unajumuisha utendaji wa kawaida ndani ya mfumo wa haki za jinai wa Cuba "na unaonesha mwelekeo wa kibinadamu wa Mapinduzi, ambayo katika tukio hili yanaendana na ukaribu wa sherehe za kidini za Juma Takatifu.”

CUBA NA VATICAN

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.

16 Machi 2026, 10:10