Cuba yawaachilia wafungwa 51 wakati wa Juma Takatifu kufuatia mazungumzo na Vatican
Vatican News
Akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari, msemaji Mkuu wa Ofisi ya vyombo vya Habari vya Vatican Bwana Matteo Bruni alithibitisha tarehe 13 Machi 2026 kwamba kumekuwa na majadiliano ya hivi karibuni kati ya Vatican na mamlaka ya Cuba "kuhusu kuachiliwa kwa wafungwa" katika Serikali ya kisiwa cha Carribean. Hii inafuatia taarifa iliyotolewa tarehe 12 Machi 2026 na maafisa wa Cuba iliyosema, "Katika moyo wa nia njema na uhusiano wa karibu na unaobadilika kati ya Serikali ya Cuba na Vatican, uhusiano ambao mawasiliano yamedumishwa kihistoria, kuhusu michakato ya mapitio na kuachiliwa kwa watu walionyimwa uhuru, Serikali ya Cuba imeamua kuwaachilia, katika siku zijazo, watu 51 walio gerezani." Taarifa hiyo pia inabainisha kuwa, wote ni wafungwa ambao wamedumisha tabia njema wakiwa gerezani kwa sehemu kubwa ya kifungo chao.
Tendo la Cuba
Serikali iliendelea kuelezea kwamba zaidi ya wafungwa 9,900 wamefaidika na msamaha tangu 2010. Iliongeza kusema kwamba "zaidi ya hayo, katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kama sehemu ya tendo la Cuba na kwa mujibu wa vifungu vya sheria, watu wengine 10,000 wanaotumikia vifungo vya gerezani wameachiliwa huru kupitia aina mbalimbali za manufaa ya kisheria."
Juma Takatifu
Hatimaye, taarifa hiyo inaelezea kwamba uamuzi huo unajumuisha utendaji wa kawaida ndani ya mfumo wa haki za jinai wa Cuba "na unaonesha mwelekeo wa kibinadamu wa Mapinduzi, ambayo katika tukio hili yanaendana na ukaribu wa sherehe za kidini za Juma Takatifu.”
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.