Tafuta

Picha ya Watoto na Papa Francisko wakati wa Siku ya Watoto Ulimwenguni katika Uwanja wa Olimpiki 2024. Picha ya Watoto na Papa Francisko wakati wa Siku ya Watoto Ulimwenguni katika Uwanja wa Olimpiki 2024.  (Vatican Media)

Papa afuta Kamati ya Siku ya Watoto Duniani

Ni kwa maandishi ya Mkono wa Papa Leo XIV yaliyochapishwa Februari 2026 kuhusu chombo kilichoanzishwa mwaka 2024 ili kuandaa na kuratibu kile kinachoitwa:"Siku za Watoto Duniani."Jukumu lote sasa linahamishiwa kwa Baraza la Kipapa la Walei,Familia na Maisha,ambapo Papa alikuwa tayari amehamisha Kamati hiyo mwezi Agosti iliyopita.Hati hiyo na sheria imefutwa kama ilivyo kwa sheria na kanuni zote zilizopitishwa hadi sasa.

Na Salvatore Cernuzio – Vatican.

Baada ya kuiweka  mnamo  mwezi Agosti iliyopita ndani ya Baraza la Walei, Familia na Maisha, na hivyo kubadilisha asili yake kama Shirika linaloripoti moja kwa moja kwa Papa, Baba Mtakatifu Leo XIV, kwa barua ya mkono wake(chirograph)iliyochapishwa Ijumaa tarehe 13 Februari 2026 amefuta Kamati ya Kipapa ya Siku ya Watoto Ulimwenguni Hiki ni chombo kilichoanzishwa na Papa Francisko mnamo Novemba 2024 kikiwa na jukumu la kusimamia "uhuishaji wa Kikanisa na Shirika la kichungaji" la kile kinachoitwa: "Siku za Vijana Duniani," tukio ambalo, baada ya Siku za Vijana Duniani, limekuwa likiwakusanya maelfu ya watoto kutoka ulimwenguni kote  kuja Roma kwa ajili ya tukio la muziki, imani, na ushuhuda.

Wajibu wa Baraza la Kipapa kwa Walei, Familia na Maisha

Mpango huu utaendelea kusherehekewa katika toleo la pili ambalo limepangwa kufanyika kunako tarehe 25-27 Septemba 2026, jijini Roma, kama ilivyotangazwa na Papa  Leo XIV mnamo  Novemba 2025. Hili "linashirikisha wasiwasi" wa Papa Francisko kwamba "Kanisa liwaangalie watoto, ikiwa ni pamoja na kuanzisha siku inayojikta kwao," Papa  Leo XIV  mwenyewe anaandika katika maandishi hayo ya mkono(Chirograph.) Hata hivyo, jukumu la kupanga na kuratibu linaelekezwa kikamilifu kwa Baraza la Kipapa lililotajwa hapo juu, linaloongozwa na Kardinali Kevin Farrell. "Baraza la Kipapa kwa Walei, Familia, na Maisha lina uwezo wa kushughulikia masuala yote yaliyopewa Kamati ya Kipapa hapo awali," inasema hati hiyo.

Kukuza ushirikiano na kazi yenye ufanisi zaidi

Papa Leo XIV, anaelezea zaidi, uamuzi huo unaendana na ule uliochukuliwa tayari na agizo jipya la mwezi Agosti 2025 na "kwa lengo la kukuza ushirikiano na kazi yenye ufanisi zaidi kwa ajili ya utekelezaji wa mpango huu mzuri, baada ya kunishauri ipasavyo." Papa Leo XIV pia anafuta kupitia  mandisho  hayo,  sheria zinazohusiana za Kamati iliyopita ya Kipapa: "Vitendo na kanuni zozote zilizopitishwa hadi sasa" na Kamati pia zinafutwa, na hazina matokeo ya kisheria katika mifumo ya kisheria na ya kiraia."

Zaidi ya hayo, rais, makamu rais, na wanachama wengine "mara moja" wanaacha kazi. Hati hiyo inasema kwamba Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la  Walei, Familia, na Maisha "atafafanua ripoti za Kamati zinazosubiriwa" na kuwasilisha "bajeti ya mwisho kwa Sekretarieti ya Uchumi kwa ajili ya kupitishwa na kwa uamuzi wowote kuhusu mgao wa mali zilizobaki."

Juma la kwanza la Siku ya Watoto Ulimwenguni (WYD) ilifanyika mnamo 25 Mei 2024, katika Uwanja wa Olimpiki jijini  Roma, mbele ya Papa Francisko na kwa ushiriki wa zaidi ya watoto na vijana 50,000, wakiwemo wale kutoka maeneo magumu na yaliyokumbwa na vita. Sasa, Baraza la Kipapa la Walei, ambalo tayari linaandaa Juma ya  WYD,  litakuwa na jukumu la tukio hilo, likishughulikia masuala yanayohusiana na walei na familia na maisha, ikiwa ni pamoja na huduma ya kichungaji na utunzaji wa watoto.

KUFUTWA KWA KAMATI YA WYD

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

13 Februari 2026, 15:10