Papa afuta Kamati ya Siku ya Watoto Duniani
Na Salvatore Cernuzio – Vatican.
Baada ya kuiweka mnamo mwezi Agosti iliyopita ndani ya Baraza la Walei, Familia na Maisha, na hivyo kubadilisha asili yake kama Shirika linaloripoti moja kwa moja kwa Papa, Baba Mtakatifu Leo XIV, kwa barua ya mkono wake(chirograph)iliyochapishwa Ijumaa tarehe 13 Februari 2026 amefuta Kamati ya Kipapa ya Siku ya Watoto Ulimwenguni Hiki ni chombo kilichoanzishwa na Papa Francisko mnamo Novemba 2024 kikiwa na jukumu la kusimamia "uhuishaji wa Kikanisa na Shirika la kichungaji" la kile kinachoitwa: "Siku za Vijana Duniani," tukio ambalo, baada ya Siku za Vijana Duniani, limekuwa likiwakusanya maelfu ya watoto kutoka ulimwenguni kote kuja Roma kwa ajili ya tukio la muziki, imani, na ushuhuda.
Wajibu wa Baraza la Kipapa kwa Walei, Familia na Maisha
Mpango huu utaendelea kusherehekewa katika toleo la pili ambalo limepangwa kufanyika kunako tarehe 25-27 Septemba 2026, jijini Roma, kama ilivyotangazwa na Papa Leo XIV mnamo Novemba 2025. Hili "linashirikisha wasiwasi" wa Papa Francisko kwamba "Kanisa liwaangalie watoto, ikiwa ni pamoja na kuanzisha siku inayojikta kwao," Papa Leo XIV mwenyewe anaandika katika maandishi hayo ya mkono(Chirograph.) Hata hivyo, jukumu la kupanga na kuratibu linaelekezwa kikamilifu kwa Baraza la Kipapa lililotajwa hapo juu, linaloongozwa na Kardinali Kevin Farrell. "Baraza la Kipapa kwa Walei, Familia, na Maisha lina uwezo wa kushughulikia masuala yote yaliyopewa Kamati ya Kipapa hapo awali," inasema hati hiyo.
Kukuza ushirikiano na kazi yenye ufanisi zaidi
Papa Leo XIV, anaelezea zaidi, uamuzi huo unaendana na ule uliochukuliwa tayari na agizo jipya la mwezi Agosti 2025 na "kwa lengo la kukuza ushirikiano na kazi yenye ufanisi zaidi kwa ajili ya utekelezaji wa mpango huu mzuri, baada ya kunishauri ipasavyo." Papa Leo XIV pia anafuta kupitia mandisho hayo, sheria zinazohusiana za Kamati iliyopita ya Kipapa: "Vitendo na kanuni zozote zilizopitishwa hadi sasa" na Kamati pia zinafutwa, na hazina matokeo ya kisheria katika mifumo ya kisheria na ya kiraia."
Zaidi ya hayo, rais, makamu rais, na wanachama wengine "mara moja" wanaacha kazi. Hati hiyo inasema kwamba Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia, na Maisha "atafafanua ripoti za Kamati zinazosubiriwa" na kuwasilisha "bajeti ya mwisho kwa Sekretarieti ya Uchumi kwa ajili ya kupitishwa na kwa uamuzi wowote kuhusu mgao wa mali zilizobaki."
Juma la kwanza la Siku ya Watoto Ulimwenguni (WYD) ilifanyika mnamo 25 Mei 2024, katika Uwanja wa Olimpiki jijini Roma, mbele ya Papa Francisko na kwa ushiriki wa zaidi ya watoto na vijana 50,000, wakiwemo wale kutoka maeneo magumu na yaliyokumbwa na vita. Sasa, Baraza la Kipapa la Walei, ambalo tayari linaandaa Juma ya WYD, litakuwa na jukumu la tukio hilo, likishughulikia masuala yanayohusiana na walei na familia na maisha, ikiwa ni pamoja na huduma ya kichungaji na utunzaji wa watoto.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here