Papa amemteua Mons.Kisito kuwa Balozi Mpya wa Vatican nchini Jamhuri ya Congo
Vatican News
Jumatano tarehe 28 Januari 2026, Baba Mtakatifu Leo XIV alimteua Monsinyo Relwendé Kisito Ouédraogo, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa Afisa wa Kitengo cha Masuala ya Jumla cha Sekretarieti ya Vatican, kuwa Balozi mpya wa Vatican katika Jamhuri ya Congo. Na wakati huo huo kumpandishwa na kuwa na makao ya Ilta, akiwa na hadhi ya Uaskofu Mkuu.
Akiwa amezaliwa huko Gourcy, nchini Burkina Faso, tarehe 9 Aprili 1972, Monsinyo Kisito alipewa Daraja Takatifu la Ipadre mnamo tarehe 13 Desemba 2000, na kwa ajili ya Jimbo la Ouahigouya. Ana shahada ya Liturujia. Alianza huduma yake katika Kitengo cha Masuala ya Jumla ya Sekretarieti ya Nchi mnamo tarehe 11 Januari 2010. Anazungumza Kifaransa, Kiingereza, Kiitaliano, na Kijerumani.
Katibu Mkuu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, ndiye aliyawatangazia kuhusu kuteuliwa kwa balozi mpya na ambaye amekuwa mshirika wa karibu naye katika miaka ya hivi karibuni, ambapo tangazo la uteuzi lilifanyika katika Maktaba ya Loggia ya Tatu, mbele ya Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher na wahudumu wa Ofisi hiyo ya Sekretarieti ya Vatican.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here