2026.01.28 Kardinali ametangaza kuteuliwa kwa Monsinyo Kisito kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Jamhuri ya Congo. 2026.01.28 Kardinali ametangaza kuteuliwa kwa Monsinyo Kisito kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Jamhuri ya Congo. 

Papa amemteua Mons.Kisito kuwa Balozi Mpya wa Vatican nchini Jamhuri ya Congo

Baba Mtakatifu Leo XIV,Januari 28 amemteua Balozi Mpya wa Vatican wa Jamhauri Congo Brazaville,Monsinyo Relwendé Kisito Ouédraogo, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa Afisa wa Kitengo cha Masuala ya Jumla ya Sekretarieti ya Vatican kwa kumwinua wakati huo huo kuwa Askofu Mkuu na Makao ya Ilta.

Vatican News

Jumatano tarehe 28  Januari 2026, Baba Mtakatifu Leo XIV alimteua Monsinyo Relwendé Kisito Ouédraogo, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa Afisa wa Kitengo cha Masuala ya Jumla cha  Sekretarieti ya Vatican, kuwa Balozi mpya wa Vatican katika Jamhuri ya Congo. Na wakati huo huo kumpandishwa na kuwa na makao ya Ilta, akiwa na hadhi ya Uaskofu Mkuu.

Monsinyo Kisito
Monsinyo Kisito

Akiwa amezaliwa huko Gourcy, nchini Burkina Faso, tarehe 9 Aprili  1972, Monsinyo Kisito alipewa Daraja Takatifu la Ipadre  mnamo tarehe 13 Desemba 2000, na kwa ajili ya Jimbo la Ouahigouya. Ana shahada ya Liturujia. Alianza huduma yake katika Kitengo cha Masuala ya Jumla ya Sekretarieti ya Nchi mnamo  tarehe 11 Januari  2010. Anazungumza Kifaransa, Kiingereza, Kiitaliano, na Kijerumani.

Katibu Mkuu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, ndiye aliyawatangazia kuhusu kuteuliwa kwa  balozi mpya na ambaye amekuwa mshirika wa karibu naye katika miaka ya hivi karibuni, ambapo tangazo la  uteuzi lilifanyika katika Maktaba ya Loggia ya Tatu, mbele ya Katibu wa  Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, Askofu Mkuu  Paul Richard Gallagher na wahudumu wa Ofisi hiyo ya Sekretarieti ya Vatican.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here

28 Januari 2026, 17:30