Tafuta

2026.01.15 Ibada ya kuweka zana za Mlango Mtakatifu kwenye ukuta za Mlango Mtakatifu wa Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta. 2026.01.15 Ibada ya kuweka zana za Mlango Mtakatifu kwenye ukuta za Mlango Mtakatifu wa Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta.  (@VATICAN MEDIA)

Zana za Milango mitakatifu ya Basilika za kipapa zawekwa ndani ya ukuta hadi Jubilei ijayo!

Kutoka katika Ofisi ya habari ya Vatican ilielezea ratiba ya ibada za kibinafsi ambapo zana zilizohusika katika Milango Mitakatifu ya Basilika nne za Kipapa zimeanza kurudishwa kufungiwa kwenye kuta kama utamaduni unavyoelekeza kunzia tarehe 14-16 Januari 2026.

Vatican News

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Kiti Kitakatifu, kufungwa katika ukuta kwa zana za  Milango Miakatifu katika Basilika za Kipapa kunakamilika Juma hili katika sherehe za kibinafsi(Januari 14-16). Zana za Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Mtakatifu Maria Mkuu, zilifungiwa Jumanne tarehe 14 Januari 2026,  saa 1 jioni saa za Ulaya. Wakati huo huo, sheherehe iliendelea Jumatano katika Basilika ya Mtakatifu Yohane huko Lateran, ikifuatiwa na siku Alhamisi tarehe 15  Januari, kwa ajili ya kuta za Mlango Mtakatifu katika Basilika ya Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta.

Ibada ya kufungia zana za Mlango Mtakatifu
Ibada ya kufungia zana za Mlango Mtakatifu   (@VATICAN MEDIA)

Ibada ya kujengea matofali katika Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Papa ya Mtakatifu Paulo Nje ya Kuta, ambao umevukwa na mamilioni ya mahujaji katika miezi ya hivi karibuni, ilifanyika jioni, ya tarehe 15 Januari 2026. Kardinali James Michael Harvey, Mkuu wa Basilika hiyo, aliongoza ibada hiyo, na baadaye akafuata  Monsinyo Ján Dubina, mbele ya Mshereheshaji Mkuu wa Liturujia za Kipapa, Askofu Mkuu Diego Giovanni Ravelli. Katika sala fupi ya ufunguzi, Kardinali aliwaombea mahujaji waliopitia Mlango Mtakatifu wakati wa Mwaka Mtakatifu, ili waweze kuhifadhi imani  ya kina ya Mtakatifu Paulo, tumaini lisilokatisha tamaa, na upendo unaodumu milele.

Ibada ya kufungia zana za Mlango Mtakatifu ukutani
Ibada ya kufungia zana za Mlango Mtakatifu ukutani   (@VATICAN MEDIA)

Ibada

Wafanyakazi kutoka Jiji la Vatican walijenga ukuta wa matofali ndani ya Basilika ili kufunga Mlango Mtakatifu. Ndani ya ukuta, kofia ya shaba, iliyotengenezwa kwa ajili ya tukio hilo, iliwekwa, ambayo juu yake imechorwa kauli mbiu za Papa Francisko, aliyefungua Jubilei ya kawaida ya 2025, na Papa Leo XIV, aliyeifunga. Chombo cha chuma chenye karatasi ya ngozi inayothibitisha kufunguliwa na kufungwa kwa Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Mtakatifu Paulo, kilichotiwa sahihi na baadhi ya waliokuwepo, kisha kikawekwa kwenye kofia.

Hii ilifuatiwa na medali ya dhahabu na fedha inayoadhimisha mwaka wa kwanza wa upapa wa Papa Leo XIV, medali ya fedha inayolingana na mwaka wa mwisho wa upapa wa Papa Francisko, medali kumi za shaba zinazoadhimisha miaka kumi kati ya Jubilei iliyopita, Jubilei ya Rehema mwaka  2016, na 2025, medali ya shaba ya Kiti kitupu (Sede Vacante) 2025, na medali ya ukumbusho ya fedha iliyoandaliwa na BasiliKa. Ufunguo wa Mlango Mtakatifu pia uliwekwa kwenye mfuko wenye kofia.

Utiwaji wa Saini
Utiwaji wa Saini   (@VATICAN MEDIA)

Hatimaye kofia (Capsa) ya shaba iliwekwa kwenye chombo cha risasi kilichounganishwa na kufungwa. Kardinali  Harvey na Askofu Mkuu Ravelli waliweka matofali mawili, hivyo kuanza awamu ya mwisho ya kazi ya uashi. Mwishowe hatua ya mwisho ilifunikwa na bamba lililochongwa msalaba. Sherehe ya uashi hu ilihitimishwa kwa  Sala ya Bwana na baraka.

Ufungaji kwenye ukuta zana za Mlango Mtakatifu
Ufungaji kwenye ukuta zana za Mlango Mtakatifu   (@VATICAN MEDIA)

Kwa nia hiyo Ibada ya mwisho na ya faragha ni Ijumaa jioni tarehe 16 Januari 2026, katika Basilika ya Mtakatifu Petro. Kwa mujibu wa utamaduni, wakati wa ibada, sanduku ya shaba yenye rekodi ya kufunga Mlango Mtakatifu, ufunguo wa Mlango, medali kadhaa za upapa za tangu kufunga Mlango Mtakatifu kwa mara ya mwisho, kuanzia 2016 hadi sasa, na  inapohitajika, medali ya ukumbusho wa Basilika, huingizwa kwenye sanduku hilo na kufungiwa kwenye ukuta.

Ibada ya ufungaji wa zana za Mwaka Mtakatifu na Mlango Mtakatifu
Ibada ya ufungaji wa zana za Mwaka Mtakatifu na Mlango Mtakatifu   (@VATICAN MEDIA)

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

 

16 Januari 2026, 10:25