Zana za Milango mitakatifu ya Basilika za kipapa zawekwa ndani ya ukuta hadi Jubilei ijayo!
Vatican News
Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Kiti Kitakatifu, kufungwa katika ukuta kwa zana za Milango Miakatifu katika Basilika za Kipapa kunakamilika Juma hili katika sherehe za kibinafsi(Januari 14-16). Zana za Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Mtakatifu Maria Mkuu, zilifungiwa Jumanne tarehe 14 Januari 2026, saa 1 jioni saa za Ulaya. Wakati huo huo, sheherehe iliendelea Jumatano katika Basilika ya Mtakatifu Yohane huko Lateran, ikifuatiwa na siku Alhamisi tarehe 15 Januari, kwa ajili ya kuta za Mlango Mtakatifu katika Basilika ya Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta.
Ibada ya kujengea matofali katika Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Papa ya Mtakatifu Paulo Nje ya Kuta, ambao umevukwa na mamilioni ya mahujaji katika miezi ya hivi karibuni, ilifanyika jioni, ya tarehe 15 Januari 2026. Kardinali James Michael Harvey, Mkuu wa Basilika hiyo, aliongoza ibada hiyo, na baadaye akafuata Monsinyo Ján Dubina, mbele ya Mshereheshaji Mkuu wa Liturujia za Kipapa, Askofu Mkuu Diego Giovanni Ravelli. Katika sala fupi ya ufunguzi, Kardinali aliwaombea mahujaji waliopitia Mlango Mtakatifu wakati wa Mwaka Mtakatifu, ili waweze kuhifadhi imani ya kina ya Mtakatifu Paulo, tumaini lisilokatisha tamaa, na upendo unaodumu milele.
Ibada
Wafanyakazi kutoka Jiji la Vatican walijenga ukuta wa matofali ndani ya Basilika ili kufunga Mlango Mtakatifu. Ndani ya ukuta, kofia ya shaba, iliyotengenezwa kwa ajili ya tukio hilo, iliwekwa, ambayo juu yake imechorwa kauli mbiu za Papa Francisko, aliyefungua Jubilei ya kawaida ya 2025, na Papa Leo XIV, aliyeifunga. Chombo cha chuma chenye karatasi ya ngozi inayothibitisha kufunguliwa na kufungwa kwa Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Mtakatifu Paulo, kilichotiwa sahihi na baadhi ya waliokuwepo, kisha kikawekwa kwenye kofia.
Hii ilifuatiwa na medali ya dhahabu na fedha inayoadhimisha mwaka wa kwanza wa upapa wa Papa Leo XIV, medali ya fedha inayolingana na mwaka wa mwisho wa upapa wa Papa Francisko, medali kumi za shaba zinazoadhimisha miaka kumi kati ya Jubilei iliyopita, Jubilei ya Rehema mwaka 2016, na 2025, medali ya shaba ya Kiti kitupu (Sede Vacante) 2025, na medali ya ukumbusho ya fedha iliyoandaliwa na BasiliKa. Ufunguo wa Mlango Mtakatifu pia uliwekwa kwenye mfuko wenye kofia.
Hatimaye kofia (Capsa) ya shaba iliwekwa kwenye chombo cha risasi kilichounganishwa na kufungwa. Kardinali Harvey na Askofu Mkuu Ravelli waliweka matofali mawili, hivyo kuanza awamu ya mwisho ya kazi ya uashi. Mwishowe hatua ya mwisho ilifunikwa na bamba lililochongwa msalaba. Sherehe ya uashi hu ilihitimishwa kwa Sala ya Bwana na baraka.
Kwa nia hiyo Ibada ya mwisho na ya faragha ni Ijumaa jioni tarehe 16 Januari 2026, katika Basilika ya Mtakatifu Petro. Kwa mujibu wa utamaduni, wakati wa ibada, sanduku ya shaba yenye rekodi ya kufunga Mlango Mtakatifu, ufunguo wa Mlango, medali kadhaa za upapa za tangu kufunga Mlango Mtakatifu kwa mara ya mwisho, kuanzia 2016 hadi sasa, na inapohitajika, medali ya ukumbusho wa Basilika, huingizwa kwenye sanduku hilo na kufungiwa kwenye ukuta.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here