Tafuta

2026.01.15 Kardinali  Parolin nchini Jamhuri ya Kuwait (@TerzaLoggia) 2026.01.15 Kardinali Parolin nchini Jamhuri ya Kuwait (@TerzaLoggia)  (@TerzaLoggia)

Kard.Parolin,Kuwait,kuimarisha uhusiano wa urafiki na ushirikiano

Katika taarifa ya pamoja,Vatican na nchi ya Peninsula ya Arabia wanasisitiza umuhimu wa maadili ya kuheshimiana na kuishi kwa amani miongoni mwa dini.Mnamo Januari 16,Katibu Mkuu wa Vatican ataongoza huko Ahmadi,sherehe ya kutangazwa kwa Kanisa la Mama Yetu wa Arabia kama Basilika Ndogo.Wakati wa ziara hiyo,mazungumzo rasmi yatafanyika na Ahmad Abdullah Al-Ahmad Al-Sabah,Waziri Mkuu wa Kuwait.

Vatican News

Nchi ya Kuwait na Kiti Kitakatifu zinakaribishana kwa ziara rasmi ya Katibu Mkuu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, kuanzia Januari 14 Januari hadi 16,2026. Wakati wa ziara hiyo, kwa taarifa ya pamoja inasisitiza kuwa mfululizo wa mazungumzo rasmi utafanyika na Sheikh Ahmad Abdullah Al-Ahmad Al-Sabah, Waziri Mkuu wa Kuwait. Sherehe kuu ya kutangazwa kwa Basilika Ndogo itafanyika Ahmadi  Ijumaa tarehe 16 Januari 2026 saa 4:00 kamili asubuhi, masaa ya huko na itaongozwa na Kardinali Parolin mwenyewe.

Ziara ya Katibu Mkuu wa Vatican, hata hivyo taarifa inabainisha kuwa inalenga kuimarisha uhusiano wa urafiki na ushirikiano ambao Kiti Kitakatifu na Nchi ya Kuwait wamedumisha tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia mwaka 1968, wakati huo Kuwait ikawa nchi ya kwanza ya Baraza la Ushirikiano la Ghuba kuanzisha uhusiano kama huo na Kiti Kitakatifu. Ziara hiyo pia inalenga kushuhudia utamaduni mrefu wa kuishi pamoja kidini ambao umekuwa ukiitambulisha Nchi ya  Kuwait ndani ya Ghuba ya Arabia.

Kanisa la Mama Yetu wa Arabia, la Kwanza Nchini humo

Ziara hii ni sehemu ya sherehe za kutangazwa kwa Kanisa la Mama Yetu wa Arabia huko Ahmadi, Kuwait, kuwa kama Basilika Ndogo. Kama Kanisa la Kikatoliki la zamani zaidi katika Nchi ya  Kuwait na eneo la Ghuba ya Arabia, taarifa hiyo inafafanua zaidi, kuwa cheo  hiki kilitolewa na Mtakatifu Papa Leo XIV mnamo tarehe 28 Juni 2025, kwa kutambua umuhimu wake wa kihistoria na kiroho katika Ghuba ya Arabia.


 

Cheo hiki cha kihistoria, cha kwanza cha aina yake katika Ghuba ya  Arabia, kinasisitiza jukumu la kipekee la Kanisa la Mama Yetu wa Arabia kama Kanisa Mama la Kuwait, likiwa Kanisa la kwanza Katoliki kujengwa nchini humo. Kanisa la awali lilijengwa mwaka 1948, na Kanisa la sasa lilikamilishwa mwaka 1957 kutokana na michango ya ukarimu ya wafadhili wa eneo hilo, ambao huduma na usaidizi wao kwa jengo la kanisa unaendelea hadi leo hii.


Uwepo wa Amani kati ya Dini

Nchi ya  Kuwait, kwa maelezo ya maandishi yanasema, linathibitisha kanuni zake thabiti za kuheshimiana na kuishi kwa amani kati ya dini, maadili ambayo yamehifadhiwa katika maadili yake tangu kuanzishwa kwake na baadaye kuorodheshwa katika Katiba yake. Ziara hii pia inaashiria tukio la kuadhimisha ziara ya kihistoria iliyofanywa na marehemu Mkuu wa Kuwait, Sheikh Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah, kwa Mrithi wa Petro mnamo tarehe 6 Mei  2010, ambayo iliashiria hatua muhimu katika maendeleo ya uhusiano kati ya Nchi ya  Kuwait na Vatican.

Ziara hii ilifanyika ndani ya mfululizo wa mazungumzo rasmi ya ngazi ya juu, ikisisitiza kujitolea kwa uongozi wa Kuwait katika kuimarisha mawasiliano na mazungumzo na Vatican, iliyotanguliwa na ziara ya Waziri Mkuu wa zamani, Sheikh Nasser Al-Mohammad Al-Ahmad Al-Sabah mwaka 2009, na kufuatiwa na ziara ya Waziri Mkuu wa zamani, Sheikh Jaber Al-Mubarak Al-Hamad Al-Sabah mwaka 2015.

Kard.Parolin Kuwait

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

 

15 Januari 2026, 16:23