Ziara ya Kardinali Parolin huko Kuwait Januari 15 na 16
Vatican News
Katibu Mkuu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin atatembelea Kuwait kuanzia tarehe 15 na 16 Januari 2026. Kulingana na programu iliyochapishwa na akaunti ya X ya Sekretarieti ya Vatican @TerzaLoggia, Kardinali baada ya ziara za heshima kwa mamlaka za kiraia mahalia siku ya Alhamisi Januari 15, atatembelea Msikiti Mkuu na Dar al Athar al Islamiyyah (Jumba la Makumbusho la Vitu vya Kale vya Kiislamu). Kisha atakutana na mapadre na watawa wa kike na kiume katika Kanisa Kuu la Familia Takatifu.
Mikutano na Sherehe
Programu hiyo pia inajumuisha Misa mbili: ya kwanza, pia Alhamisi hiyo, katika Kanisa Kuu la Familia Takatifu kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 65 ya kuwekwa wakfu kwa Kanisa hilo.
Siku ya Ijumaa Januari 16
Siku ya pili, Ijumaa tarehe 16 Januari, ataadhimisha katika Basilika Ndogo ya Mama Yetu wa Arabia huko Ahmadi, wakati wa kuinuliwa kwake kuwa Basilika Ndogo ya Vikariate ya Kitume ya Arabia Kaskazini, ambayo inajumuisha, pamoja na Kuwait, Bahrain, Qatar na Saudi Arabia.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here