Tafuta

2026.07.05 Papa ameanza kipindi cha mapumzko huko Castel Gandolfo. 2026.07.05 Papa ameanza kipindi cha mapumzko huko Castel Gandolfo.  (@VATICAN MEDIA )

Papa Leo XIV huko Castel Gandolfo:kipindi cha mapumziko,sala na mazoezi

Baba Mtakatifu Leo XIV,Dominika Julai 5,mara baada ya kufika kwenye majumba ya Kirumi alichungulia kutokea dirisha la Jumba la Kitume ili kuwasalimu waamini waliokuwa wakimsubiri katika Uwanja wa Uhuru.Aliwashukuru kwa makaribisho na kuwaeleza umuhimu wa kukutana kati ya kaka na dada

Vatican News

Bango lililofunikwa juu ya kwenye balcony ya Jumba la Kitume lilitangaza kuwasili kwa Papa Leo XIV kwa waamini waliokusanyika katika uwanja wa Castel Gandolfo. Baada ya ziara ya kichungaji ya Jumamosi tarehe 4 Julai 2026 huko Lampedusa na Sala ya Malaika wa Bwana Dominika tarehe 5 Julai  katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Baba Mtakatifu Leo XIV, alasiri alikwenda  hadi mji mwingine wa Lazio mahali palipo na Jumba la Kipapa. Huko Papa atapumzika hadi Jumatatu tarehe 27 Julai kama ilivyotangazwa katika taarifa kutoka kwa Nyumba ya Kipapa.

Papa akipunga mkono wa salamu kutokea kwenye dirisha  kubwa la Jumba la Kitume la Castel Gandolfo
Papa akipunga mkono wa salamu kutokea kwenye dirisha kubwa la Jumba la Kitume la Castel Gandolfo   (@VATICAN MEDIA)

Mkutano daima ni wakati muhimu

Akiwa kwenye dirisha kubwa  la Jengo la makazi yake, alitoa maneno machache ili kurudisha furaha ya wakazi wa eneo hilo waliokuwa wakimsubiri kwa hamu kwa mwezi wa Julai, ambao kwa kawaida hutengwa kwa mapumziko kutoka ahadi zake.

Habari za jioni na  jioni njema, Castel Gandolfo! haya yalikuwa maneno ya kwanza ya Papa. Asante. Ninafurahi sana kuwa hapa miongoni mwenu, kuweza kutumia Juma chache zijazo kwa kupumzika, kusali, kusoma, na pengine michezo hapa Castel Gandolfo! Mkutano daima ni wakati muhimu, kwa hivyo ninafurahi kwamba nyote mko hapa. Asante kwa makaribisho, asante kwa kuwa kaka na dada.


Sala ya Papa

Mbele ya umati uliokuwa ukipiga kelele  ya kumkaribisha "Karibu" na kupiga makofi, Papa Leo XIV alitoa baraka zake, huku akiwaalika kukutana nao katika sala ya Malaika wa Bwana Domika ijayo na  labda "wakati mwingine."

Nawahakikishia maombi yangu, daima, lakini hasa katika juma zijazo...Mungu awe nanyi daima!

A Castel Gandolfo Leone XIV trascorrerà un periodo di riposo

Huko  Castel Gandolfo Papa Leo XIV atapumzika hadi Julai 27 (@Vatican Media)

Papa  Leo XIV alimsalimia Padre wa Parokia na Parokia ya Mtakatifu  Tommaso wa Villanova, ambapo aliadhimisha Misa mnamo tarehe 13 Julai 2025. Katika kipindi hiki cha mapumziko, Katekesi  zote zimesimamishwa, ambazo zitaanza tena Jumatano, tarehe 5 Agosti 2026, pamoja na mikutano ya kibinafsi na maalum. Wakati sala ya Malaika wa Bwana, ijayo itafanyika katika Uwanja wa "Pizza della Libertà yaani 'Uwanja wa Uhuru' huko  Castel Gandolfo,"

I fedeli in Piazza della Libertà per salutare il Papa

Waamini wakiwa katika Uwanja wa Uhuru wakimsalimia Papa(@VATICAN MEDIA)

mapumziko ya Papa Leo XIV huko Castel Gandolfo

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

06 Julai 2026, 09:10