Tafuta

Papa Leo XIV huko Castel Gandolfo Picha kutoka pango hifadhi. Papa Leo XIV huko Castel Gandolfo Picha kutoka pango hifadhi.  (foto di padre Bruno Silvestrini)

Papa Leo anahamia Castel Gandolfo kwa mwezi Julai

Kutoka Nyumba ya Kipapa imetoa taarifa kuwa kuanzia tarehe 5 Julai,Papa atahamia manispaa ya Lazio hadi tarehe 27 Julai.Katekesi zimesitisishwa na sala ya Malaika wa Bwana itafanyika katika Uwanja wa Uhuru kwa mwezi Julai.

Vatican News

Kama ilikuwa mwaka 2025, Papa Leo XIV  amechagua makazi yake huko Castel Gandolfo kwa ajili ya mapumziko yake. "Mchana huu, Dominika tarehe 5 Julai 2026,  "Baba Mtakatifu atahamia kwenye Jumba la Kitume la Castel Gandolfo kwa kipindi cha mapumziko, hadi Jumatatu, Julai 27," taarifa kutoka Nyumba ya Kipapa ilibainisha.

Taarifa hiyo ilibainisha kuwa katika kipindi hiki, Mikutano yote na katekesi inabaki imesimamishwa, na zitaanza tena Jumatano, tarehe 5 Agosti 2026. Mikutano ya kibinafsi na maalum pia inasimamishwa. Siku za Dominika kwa mwezi Julai, katika sala ya Malaika wa Bwana itakuwa katika Uwanja wa Uhuru(Piazza della Liberta,) Castel Gandolfo.

Mapumziko 2025

Mwaka 2025, Papa Leo XIV alitumia siku 16 za mapumziko katika nyumba ya Kipapa ya Villa Barberini huko Castel Gandolfo, kuanzia Julai 6 hadi 22. Katika kipindi hicho, pia alifanya mikutano kadhaa ya umma, ikiwa ni pamoja na sherehe kwenye "Borgo Laudato si'" kwa ajili ya liturujia ya kwanza ya Uhifadhi wa Uumbaji, na kisha katika Parokia ya kipapa ya Mtakatifu Tommaso wa Villanova na Kanisa Kuu la Albano.

Kipindi hicho pia kilioneshwa na mikutano kadhaa, ikiwemo mmoja na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, aliyepokelewa huko Villa Barberini, na mazungumzo ya simu na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu kufuatia shambulio la jeshi la Israeli kwenye Kanisa la Familia Takatifu huko Gaza. Baadaye Papa Leo XIV  alifanya mazungumzo ya simu na Mahmoud Abbas, Rais wa Serikali ya  Palestina.

Papa mara baada ya Angelus Julai 5

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku.  Just click here.

05 Julai 2026, 12:53