Ndege ya Papa Leo XIV imetua Roma na kuhitimisha hija yake nchini Hispania!
Vatican News
Kufuatia na hitilafu ya Injini kwenye ndege ya Iberia Airbus A320 ambayo ilitakiwa kumrudisha Roma kutoka Tenerife, Papa Leo XIV aliruka hadi Roma kwa ndege ya Mfalme wa Hispania, iliyotolewa kwa ukarimu na Mfalme huyo. Ndege hiyo ya kijeshi aina ya Falcon iliyotolewa na Mfalme Philip VI, ikiwa imembeba Papa na msafara wake wa karibu, ilitua katika Uwanja wa Ndege wa Fiumicino jijini Roma. Dakika chache baadaye, Papa alirudi Vatican kwa gari. Ndege iliondoka saa 12:05 jioni (saa 1:05 jioni nchini Italia). Wafanyakazi wa Vatican na waandishi wa habari kwenye ndege ya Papa, wanarudi Italia kwa ndege nyingine iliyotolewa na shirika hilo la IBERIA kwa mujibu wa Ofisi ya Habari ya Vatican.
Telegramu kwa wakuu wa nchi
Wakati Papa Leo XIV alipokuwa akiruka juu ya anga, telegramu zilitumwa kwa wakuu wa nchi za Hispania na nchi nyingine: Kwa Mfalme Philip VI, Papa alitoa shukrani zake tena kwa mfalme, "kwa mamlaka na watu wa Hispania kwa mapokezi ya joto na ukarimu mkubwa walionipa wakati wa ziara hii." Akimhakikishia mfalme na Hispania yote kuhusu maombi yake ya kuendelea kwa amani na umoja wa taifa, Papa Leo XIV aliwaombea baraka nyingi za kimungu kila mmoja wao.
Kwa Mfalme Mohammed VI wa Morocco na watu wake, Papa alirudia matashi yake mema, akiwahakikishia maombi yake "kwa ajili ya mema ya Ufalme."
Kwa Rais wa Italia Sergio Mattarella, Papa aliandika kwamba nchini Hispania alikuwa na furaha "ya kupata imani hai ya watu hao wapendwa ambao, wenye mizizi katika maadili ya kiinjili, bado leo wanasimama kwa roho yao ya ukaribishaji na udugu wa Kikristo." Na aliwahakikishia kuhusu maombi yake ya kila mara "kwa ajili ya taifa pendwa la Italia."
Kukosa Mkutano wa Waandishi wa Habari
Katika safari ya ndege ya kilomita 3,036 ya kuja Roma, iliyopangwa kuchukua saa 4 na dakika 40, mkutano wa kiutamaduni wa waandishi wa habari 80 waliosindikiana na Papa katika hatua zote za safari yake, kutoka Madrid hadi Barcelona, kutoka Kisiwa cha Kanari hadi Tenerife, haukufanyika.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here
