Tafuta

Safari ya Papa Leo XIV kurudi Roma na ndege ya Mfalme Philip wa Hispania

Kutokana na tatizo la kiufundi la ndege aina ya Iberia Airbus A320 katika Uwanja wa Ndege wa Tenerife,Papa Leo XIV aliondoka huko kuja Roma kwa ndege ya Mfalme wa Hispania,(Falcon ya kijeshi,)saa 12:08 jioni(saa za huko) na atawasili Roma ifikapo saa 5:00 usiku(saa za Roma).Wafanyakazi wa Vatican na waandishi wa habari,watarudi katika saa zijazo kwa ndege nyingine iliyotolewa na shirika la Iberia.

Vatican News

Kufuatia na hitilafu ya Injini kwenye ndege aina ya Iberia (Airbus A320) ambayo ilitakiwa kumrudisha Roma kutokaTenerife, Papa Leo XIV anarudi Roma akiwa na Falcon ya kijeshi ya Mfalme wa Hispania, iliyotolewa kwa utashi na Mfalme huyo. Ndege hiyo iliondoka saa 12:08 jioni (saa 1:08 jioni nchini Italia) na itawasili Roma yapata saa 5:00 usiku(saa za Roma), kulingana na Ofisi ya Habari ya Vatican. Wafanyakazi wa Vatican na waandishi wa habari waliokuwa kwenye ndege ya Papa watarudi katika saa chache zitakazofuata kwa ndege nyingine iliyotolewa na IBERIA.

Papa na Mfalme wakitelemka kutoka kwenye ndege
Papa na Mfalme wakitelemka kutoka kwenye ndege   (@Vatican Media)

Kushuka kwa Papa kutoka kwenye ndege ya kwanza

Kwa hivyo, baada ya siku saba, Ziara ya nne ya kimataifa ya kitume ya Baba Mtakatifu  Leo XIV katika Uwanja wa Ndege wa Tenerife Norte - Los Rodeos,  ilimalizika kwa njia isiyo ya kawaida ya ziara yake  iliyompeleka Hispania kuanzia Juni 6 hadi 12. Kuondoka kulicheleweshwa kwa muda mrefu kutokana na tatizo la kiufundi na Injini ya ndege ya Iberia Airbus A320. Mchakato wa kupaa ulianza yapata saa 10:15 jioni kwa saa za huko (saa 11:15 jioni kwa saa za Italia), tayari ikiwa imechelewa kwa zaidi ya saa moja. Muda mfupi baadaye, ngazi zilirudishwa, na Papa alisindikizwa kurudi kwenye sebule ya VIP ya uwanja wa ndege na Mfalme Philip VI, ambaye alikuwa amemuaga muda mfupi. Muda mfupi baadaye, Katibu wa  Vatican, Kardinali Pietro Parolin, na Makadinali na maaskofu wengine katika msafara wa Papa pia walishuka.

Kardinali, Papa na washiriki wachache katika ndege ya kifalme
Kardinali, Papa na washiriki wachache katika ndege ya kifalme   (@Vatican Media)

Hafla ya kuaga

Hata hivyo baada ya maadhimisho ya misa, alipofika uwanja wa ndege yapata saa 9:45 alasiri kwa saa za huko, Papa Leo XIV alilakiwa na Mfalme Philip VI wa Hispania, mamlaka kadhaa mahalia, na ujumbe wa Kanisa la eneo hilo. Baada ya kuimbwa kwa nyimbo za taifa na heshima kwa bendera, Papa Leo XIV  na Mfalme walipitia Walinzi wa Heshima na kisha wakawasalimu wajumbe wao. Miongoni mwa mamlaka za Hispania zilizokuwepo kwenye lami walikuwa msemaji wa Serikali na Waziri wa Ujumuishi, Usalama wa Jamii, na Uhamiaji, Elma Saiz, na Gavana wa Visiwa vya Kanari, Fernando Clavijo. Hao wote walikuwa chini ya ngazi za ndege, na Mfalme baada ya kuaga wakisubiri ndege iondoke lakini haikuwa hivyo.

Ndege ya kijeshi ya Mfalme wa Hispania ikapaa kumrudisha Papa Roma
Ndege ya kijeshi ya Mfalme wa Hispania ikapaa kumrudisha Papa Roma   (@Vatican Media)

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

12 Juni 2026, 20:30