Siku ya kumi ya Papa Leo XIV barani Afrika
Joseph Tulloch-Bata,Guinea ya Ikweta na Angella Rwezaula-Vatican.
Siku nzima ya mwisho ya Papa Leo XIV barani Afrika ilifikia kikomo cha ushairi mzuri sana, Jumatano usiku, huku uwanja uliojaa vijana wakiimba na kucheza chini ya mvua kubwa ya kitropiki. Makumi ya maelfu kadiri ya makisio wapatao 50,000 hivi, walikuwa wamekusanyika katika uwanja wa mpira wa miguu huko Bata, katika jiji kubwa zaidi la Guinea ya Ikweta, kwa ajili ya mkutano wa Papa na vijana na familia. Kisha mbingu zikafunguka za mvua kubwa.
Huku baadhi wakikimbilia kujificha chini ya paa la uwanja, wengine walikaa chini ya mvua kubwa, wakicheza pamoja katika kundi kubwa huku wakisubiri kuwasili kwa Papa. Hali ya hewa katika uwanja huo, tayari ilikuwa ya radi, ilifikia kiwango cha juu zaidi wakati Papa Leo XIV alipojitokeza. Shangwe kubwa zilisikika si tu kwa Papa, bali pia kwa wenyeji waliopanda jukwaani pamoja naye kushirikisha historia za imani yao na kucheza ngoma za kitamaduni.
Katika hotuba yake, Papa aliwaambia wale waliokusanyika kwamba "mwanga mkali zaidi hapa ni ule unaong'aa machoni mwenu, kwenye nyuso zenu, katika tabasamu zenu na kupitia nyimbo zenu." Aliwahimiza wasikilizaji wake "daima kuweka mfano wa maelewano miongoni mwenu," na kuonesha kupitia matendo yao kwamba "furaha kubwa zaidi, katika kila hali, hutokana na kujua jinsi ya kutoa."
Hakuna aliyetengwa na upendo wa Mungu
Mvua ilianza mapema siku hiyo, wakati Papa Leo XIV alipokuwa akitembelea gereza la Bata. Ilianza kama matone madogo, ikaanza kunyesha kwa nguvu ndani ya dakika chache. "Katika baadhi ya maeneo," Papa alisema kabla ya kusoma hotuba yake iliyoandaliwa, "inasemekana kwamba mvua ni ishara ya baraka za Mungu. Tuombe kwamba hii iwe hivyo kweli."
Gereza la Bata linajulikana kwa hali yake ngumu. Wafungwa waliokutana na Papa walilazimishwa kusimama katika safu nadhifu, wakiwa na vichwa vilivyonyolewa na suti za kuruka ambazo rangi zao zilitofautiana kulingana na uhalifu ambao walikuwa wamefungwa.
"Hakuna mtu aliyetengwa na upendo wa Mungu," Papa aliwaambia wafungwa waliokusanyika. "Kila mmoja wetu, pamoja na histroia zetu za kipekee, makosa na mateso, anabaki kuwa wa thamani machoni pa Bwana."
'Njaa' kwa ajili ya mustakabali wenye matumaini
Mapema siku hiyo hiyo, Papa Leo XIV alikuwa ametembelea Mongomo, jiji lililoko mashariki mwa Guinea ya Ikweta, kwenye mpaka na Gabon.
Huko, aliadhimisha Misa katika Kanisa Kuu la Bikira Mkingiwa dhambi ya Asili Kanisa la pili kwa ukubwa barani Afrika. Fataki zenye rangi za bendera ya Ikweta ziliinuka kutoka kwenye nguzo kumlaki alipofika, na umati wa watu waliofika makumi ya maelfu walishangilia na kupungia mkono.
Hapo awali mji wa mpakani uliokuwa mtulivu, Mongomo ulibadilishwa na ugunduzi wa mafuta katika miaka ya 1990 - lakini, kama mahali pengine nchini, utajiri mpya uliopatikana ulibaki mikononi mwa wachache waliochaguliwa.
Katika mahubiri yake, Papa alibainisha kwamba Mungu alikuwa ameipatia Guinea ya Ikweta "utajiri mkubwa wa asili," na akawasihi wasikilizaji wake kufanya kazi pamoja ili kuifanya iwe "baraka kwa wote."
Katika Guinea ya Ikweta, alisema, kuna "njaa ya mustakabali uliojaa matumaini," lakini, alisisitiza, huu sio mustakabali ambao tunaweza "kuusubiri tu," bali ni ule ambao "sisi wenyewe tumeitwa kuujenga kwa neema ya Mungu."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.
