Siku ya kumi ya Papa Leo XIV barani Afrika

Katika siku yake ya mwisho ya Ziara yake ya Kitume barani Afrika,Papa Leo XIV aliadhimisha Misa katika Kanisa la pili kwa ukubwa barani humo,alitembelea wafungwa na kuwaeleza "hakuna mtu aliyetengwa na upendo wa Mungu", na hatimaye aliwaona vijana wa Bata wakicheza kwenye mvua kwa shagwe kuu.Haya na mengine ni katika picha.

Joseph Tulloch-Bata,Guinea ya Ikweta na Angella Rwezaula-Vatican.

Siku nzima ya mwisho ya Papa Leo XIV barani Afrika ilifikia kikomo cha ushairi mzuri sana, Jumatano usiku, huku uwanja uliojaa vijana wakiimba na kucheza chini ya mvua kubwa ya kitropiki. Makumi ya maelfu kadiri ya makisio wapatao 50,000 hivi, walikuwa wamekusanyika katika uwanja wa mpira wa miguu huko Bata, katika jiji kubwa zaidi la Guinea ya Ikweta, kwa ajili ya mkutano wa Papa na vijana na familia. Kisha mbingu zikafunguka za mvua kubwa.

Vijana katika Uwanja wa Bata
Vijana katika Uwanja wa Bata   (@Vatican Media)

Huku baadhi wakikimbilia kujificha chini ya paa la uwanja, wengine walikaa chini ya mvua kubwa, wakicheza pamoja katika kundi kubwa huku wakisubiri kuwasili kwa Papa. Hali ya hewa katika uwanja huo, tayari ilikuwa ya radi,  ilifikia kiwango cha juu zaidi wakati Papa Leo XIV alipojitokeza. Shangwe kubwa zilisikika si tu kwa Papa, bali pia kwa wenyeji waliopanda jukwaani pamoja naye kushirikisha historia za imani yao na kucheza ngoma za kitamaduni.

Papa aliwafikia baada ya kuwazungukia katika uwanja wa Bata
Papa aliwafikia baada ya kuwazungukia katika uwanja wa Bata   (@Vatican Media)

Katika hotuba yake, Papa aliwaambia wale waliokusanyika kwamba "mwanga mkali zaidi hapa ni ule unaong'aa machoni mwenu, kwenye nyuso zenu, katika tabasamu zenu na kupitia nyimbo zenu." Aliwahimiza wasikilizaji wake "daima kuweka mfano wa maelewano miongoni mwenu," na kuonesha kupitia matendo yao kwamba "furaha kubwa zaidi, katika kila hali, hutokana na kujua jinsi ya kutoa."

Wakati wa hotuba yake
Wakati wa hotuba yake   (@Vatican Media)

Hakuna aliyetengwa na upendo wa Mungu

Mvua ilianza mapema siku hiyo, wakati Papa Leo XIV alipokuwa akitembelea gereza la Bata. Ilianza kama matone madogo, ikaanza kunyesha kwa nguvu ndani ya dakika chache. "Katika baadhi ya maeneo," Papa alisema kabla ya kusoma hotuba yake iliyoandaliwa, "inasemekana kwamba mvua ni ishara ya baraka za Mungu. Tuombe kwamba hii iwe hivyo kweli."

Papa alitazama na kufurahi ngoma ya vijana
Papa alitazama na kufurahi ngoma ya vijana   (@Vatican Media)

Gereza la Bata linajulikana kwa hali yake ngumu. Wafungwa waliokutana na Papa walilazimishwa kusimama katika safu nadhifu, wakiwa na vichwa vilivyonyolewa na suti za kuruka ambazo rangi zao zilitofautiana kulingana na uhalifu ambao walikuwa wamefungwa.

Kwa wafungwa Papa aliwambia hakuna anayetengwa na upendo wa Mungu
Kwa wafungwa Papa aliwambia hakuna anayetengwa na upendo wa Mungu   (@Vatican Media)
Wafungwa wakiwa mstarini
Wafungwa wakiwa mstarini   (@Vatican Media)

"Hakuna mtu aliyetengwa na upendo wa Mungu," Papa aliwaambia wafungwa waliokusanyika. "Kila mmoja wetu, pamoja na histroia zetu za kipekee, makosa na mateso, anabaki kuwa wa thamani machoni pa Bwana."

Wafungwa walimzawadia Papa Msalaba
Wafungwa walimzawadia Papa Msalaba   (@Vatican Media)

'Njaa' kwa ajili ya mustakabali wenye matumaini

Mapema siku hiyo hiyo, Papa Leo XIV alikuwa ametembelea Mongomo, jiji lililoko mashariki mwa Guinea ya Ikweta, kwenye mpaka na Gabon.

Misa huko Mongomo
Misa huko Mongomo   (@Vatican Media)
Misa huko Mongomo
Misa huko Mongomo   (@Vatican Media)
Wanakwaya katika Misa huko Mongomo
Wanakwaya katika Misa huko Mongomo   (@Vatican Media)

Huko, aliadhimisha Misa katika Kanisa Kuu la Bikira Mkingiwa dhambi ya Asili  Kanisa la pili kwa ukubwa barani Afrika. Fataki zenye rangi za bendera ya Ikweta ziliinuka kutoka kwenye nguzo kumlaki alipofika, na umati wa watu waliofika makumi ya maelfu walishangilia na kupungia mkono.

Fataki za Rangi ya Bendera ya Guinea Ikweta na Vatican
Fataki za Rangi ya Bendera ya Guinea Ikweta na Vatican   (@Vatican Media)
Fataki za rangi
Fataki za rangi   (@Vatican Media)

Hapo awali mji wa mpakani uliokuwa mtulivu, Mongomo ulibadilishwa na ugunduzi wa mafuta katika miaka ya 1990 - lakini, kama mahali pengine nchini, utajiri mpya uliopatikana ulibaki mikononi mwa wachache waliochaguliwa.

Basilika ya Bikira Maria Mkingiwa huko Mongomo
Basilika ya Bikira Maria Mkingiwa huko Mongomo   (@Vatican Media)

Katika mahubiri yake, Papa alibainisha kwamba Mungu alikuwa ameipatia Guinea ya Ikweta "utajiri mkubwa wa asili," na akawasihi wasikilizaji wake kufanya kazi pamoja ili kuifanya iwe "baraka kwa wote."

Umati ulimsubiri Papa huko Mongomo
Umati ulimsubiri Papa huko Mongomo   (@Vatican Media)

Katika Guinea ya Ikweta, alisema, kuna "njaa ya mustakabali uliojaa matumaini," lakini, alisisitiza, huu sio mustakabali ambao tunaweza "kuusubiri tu," bali ni ule ambao "sisi wenyewe tumeitwa kuujenga kwa neema ya Mungu."

Papa alirusha Rozari iliyotenegezwa kwa maputo
Papa alirusha Rozari iliyotenegezwa kwa maputo   (@Vatican Media)

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

22 Aprili 2026, 21:49