Tafuta

Papa Leo XIV:Mambo muhimu katika Mkutano na Vijana na Familia,Aprili 22!

"Mwanga angavu zaidi sasa ni ule wa macho yenu,nyuso zenu;tabasamu zenu,nyimbo zenu,ngoma zenu:kila kitu kinashuhudia kwamba Kristo ni furaha,maana,msukumo na uzuri wa maisha yetu."Ni sifa aliyotoa Papa Leo XIV kwa umati wa vijana na familia katika Uwanja wa Bata nchini Guinea ya Ikweta,Jumatano jioni tarehe 22 Aprili.Katika Picha unaweza kuona furaha ya mapokezi na mkutano huo.

Na Angella Rwezaula-Vatican.

Katika mkutano wake wa  mwisho barani Afrika, akiwa katika Hija ya Kitume baada ya kuanzia na Algeria, Cameroon, Angola na hatimaye Guinea ya Ikweta, Baba Mtakatifu leo XIV, baada ya siku yake kali kweli kweli aliweza kusikiliza ushuhuda wa Vijana na familia za Guinea ya Ikweta,  waliokusanyika katika Uwanja wa Bata. Licha ya mvua iliyonyeshe nyingi  hawakujali  vijana wa Guinea ya Ikweta  na wazazi wao, Jumatano tarehe 22 Aprili 2026. Zifuatazo ni picha zinazoonesha tukio hilo la kusisimua.

Askofu alianza kuzungumza kwanza
Askofu alianza kuzungumza kwanza   (@Vatican Media)
Umati Mkubwa wa vijana na familia
Umati Mkubwa wa vijana na familia   (@Vatican Media)
Zawadi mbali mbali za kiutamaduni
Zawadi mbali mbali za kiutamaduni   (@Vatican Media)

Kuanzia changamoto za wanawake mahali pa kazi hadi zile zinazotokana na ndoa, ambazo hukua katika uhuru, Baba Mtakatifu Leo XIV katika hotuba yake  mara baada ya kusikiliza shuhuda mbali mbali alisisitiza umuhimu wa kulinda maadili ya familia, hata wakati hukumu, ubaguzi, na dhana potofu zinapojaribu kuyadhoofisha.

Zawadi mbali mbali za kiutamaduni
Zawadi mbali mbali za kiutamaduni   (@Vatican Media)

Papa alisema "Kila kitu huchangia urithi  wa mng'ao na wenye changamoto, ambao vizazi vipya vinaitwa kuuunga mkono na kuujenga."

Zawadi za kiutamaduni
Zawadi za kiutamaduni   (@Vatican Media)

"Maisha yaliyotolewa kwa Mungu ni ya furaha, lakini lazima yafanywe upya kila siku kupitia sala, sakramenti na muda unaotumika na ndugu na dada ambao Bwana anawaweka njiani mwetu. Katika ushirika wa mioyo na katika matendo ya wema kwa wale wanaohitaji, miujiza ya upendo hufanywa upya kila mara," Papa alibainisha.

Papa miongozi mwa umati
Papa miongozi mwa umati   (@Vatican Media)

"Wapendwa, mmekuja kwenye mkutano huu pamoja na familia zenu. Ni udongo wenye rutuba ambapo ukuaji wenu wa kibinadamu na Kikristo, kama mti mchanga na dhaifu, huzama mizizi yake. Basi, ninawaalika kumshukuru Bwana pamoja kwa zawadi ya wapendwa wenu."

Vijana kwa furaha kubwa
Vijana kwa furaha kubwa   (@Vatican Media)
Mkutano wa Papa na vijana na familia
Mkutano wa Papa na vijana na familia   (@Vatican Media)

"Wengi wenu mtajiandaa kupokea sakramenti ya Ndoa Takatifu. Kuwa wanandoa na wazazi ni dhamira ya kusisimua, agano la kuishi siku baada ya siku. Ndani ya agano hili, mtagunduana upya kila mara mnaposhirikiana na Mungu katika muujiza wa maisha na katika kujenga furaha kwa ajili yenu na kwa ajili ya watoto wenu."

Ngoma ya kiutamaduni
Ngoma ya kiutamaduni   (@Vatican Media)
Ngoma za kiutamaduni
Ngoma za kiutamaduni   (@Vatican Media)

"Kuweni tayari kukubali wito huu kama safari ya upendo wa kweli unaokua katika uhuru; kama safari ya matumaini, inayotokana na ufahamu kwamba Mungu hatakuacha kamwe; na kama safari ya utakatifu, ambapo daima unatafuta mema na furaha ya wengine."

Furaha ya maisha katika Kristo
Furaha ya maisha katika Kristo   (@Vatican Media)

"Familia inayojua jinsi ya kukaribisha na kupenda inakuwa chanzo cha mwanga na joto. Papa Francisko anaielezea familia vizuri kwa maneno haya: “Baba na mama, wanandoa wenye historia yao binafsi ya upendo… wanandoa wanaopenda na kuzaa maisha ni alama ya kweli na iliyo hai… inayoweza kumfunua Mungu Muumba na Mwokozi” (Wosia wa Kitume Amoris Laetitia, 9, 11)."

Wanaonekana mapadre nyuma ya watoto na vijana
Wanaonekana mapadre nyuma ya watoto na vijana   (@Vatican Media)
Familia inayosubiri maisha mapya
Familia inayosubiri maisha mapya   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu alisema, "Wapendwa vijana, wazazi na wote waliopo, hebu tuhamasishwe na uzuri wa upendo; hebu tuwe mashahidi wa upendo ambao Yesu ametupa na kutufundisha!"

Papa akiwatazama wanae wa Afrika
Papa akiwatazama wanae wa Afrika   (@Vatican Media)
Taifa la Mungu
Taifa la Mungu   (@Vatican Media)

"Tuoneshe kila siku kwamba ni vizuri kupenda,  kwamba furaha kubwa zaidi, katika kila hali, hutokana na kujua jinsi ya kutoa na kujitoa wenyewe, hasa tunapowafikia wale wanaohitaji zaidi. Nuru ya upendo, inayohamasishwa katika nyumba zetu na kuishi kwa imani, inaweza kubadilisha ulimwengu,  hata miundo na taasisi zake, ili kila mtu aheshimiwe na pasiwepo mtu anayesahaulika.

Papa aliwaaga
Papa aliwaaga   (@Vatican Media)
Shuhuda mbali mbali
Papa akiwa anazungumza
Papa akiwa anazungumza   (@Vatican Media)

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

22 Aprili 2026, 21:02