Papa Leo XIV:Lazima kuhudumia ubinadamu wenye kiu ya ukweli na haki!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV alitoa tafakari yake Dominika ya III ya Kipindi cha Kwaresima tarehe 8 Machi 2026 kwa waamini na mahujaji waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, katika Siku ambayo inawakumbuka na kuwaenzi Wanawake, ambapo amejikita na masuala matatu, kwamba Yesu ni jibu la kiu zetu, Kanisa lazima litafute unyeti na uwajibikaji na hatimaye Kanisa lazima kuhudumia ubinadamu ulio na kiu ya ukweli na haki.
Akianza tafakari yake Baba Mtakatifu Leo XIV alisema: “Kaka na dada, Dominika Njema! Mazungumzo kati ya Yesu na Mwanamke Msamaria, uponyaji wa kipofu tangu kuzaliwa na ufufuko wa Lazzaro, tangu karne za kwanza za historia ya Kanisa, inaakisi safari ya yule ambaye wakati wa Pasaka, atapokea Ubatizo na kuanza maisha mapya.”
Kurasa za Dominika hii kwa ajili ya wakatekumeni na jumuiya nzima
Kurasa hizi kubwa za kiinjili, ambazo tunasoma kuanzia Dominika hii, zimetolewa kwa wakatekumeni, na wakati huo huo, zinasikilizwa kwa Jumuiya nzima, kwa sababu zinasaidia kuwa wakristo au ikiwa ni wakristo tayari, kuwa wa kweli zaidi na furaha zaidi. Yesu kwa hakika ni jibu la Mungu katika kiu yetu. Kama anavyoshauri Msamaria, Mkutano na Yeye unaibua ndani ya kina cha kila mtu, “chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele (Yh 4,14). Papa Leo alisisitiza kwamba “Ni watu wangapi ulimwenguni kote, wanatafuta hata leo hii chemichemi hii ya kiroho! “Wakati mwingine ninaweza kuyafikia, aliandika kijana Etty Hillesum katika shajara lake, na mara nyingine yamefunikwa na mawe na mchanga: kwa hiyo Mungu amezikwa. Na hivyo lazima kumfukua kwa upya.”
Kwaresima ni zawadi, tunaingia Juma la Tatu
Kwa kuongezea Baba Mtakatifu Leo XIV alisema “Wapendwa hakuna nguvu iliyotumiwa vizuri zaidi kama ile ambayo tunajikita kukomboa moyo. Kwa sababu hiyo, Kwaresima ni zawadi: tunaingia katika Juma la Tatu na tunaweza kusema kwa hiyo kwamba safari sasa inakuwa ya kina! Katika Injili imeandikwa hata walipofika Mitume wake na walishangaa kwamba Yesu alikuwa akizungumza na mwanamke” (Yh 4,27). Ilikuwa ngumu kwao kusikia kama utume wake kabisa, na kwamba Mwalimu alikuwa awachochee: “Hamsemi ninyi, Bado miezi minne, ndipo yaja mavuno? Tazama, mimi nawaambieni, Inueni macho yenu myatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha kuwa meupe, tayari kwa mavuno,”(Yh 4,35).
Bwana anasema inua macho yake utambue mshangao wa Mungu
Bwana anasema tena katika Kanisa lake “Inua macho na utambue mshangao wa Mungu”! Katika mashamba, miezi minne kabla ya mavuno, huwezi kuona karibu kitu chochote. Lakini pale ambapo sisi hatuoni kitu, Neema tayari inatenda, na matunda yako tayari ya kuvuna. Baba Mtakatifu aliendelea kusema kuwa “ Shamba ni kubwa: lakini watenda kazi ni wachache , kwa sababu wanaangaika na mambo mengine. Yesu kinyume chake yuko makini. Mwanamke yule Msamaria, akiwa katika ukawaida, kwa urahisi alikuwa amdharau; kinyume chake Yesu anazungumza naye, anamsikiliza, anamjali bila sababu yoyote, na bila dharau.
Ni wangapi wanatamani kuona unyeti huu katika Kanisa
Papa Leo XIV aliongeza kusema kuwa “Ni watu wangapi wanatafuta unyeti huu sawa katika Kanisa. Uwezekano huu! Na jinsi gani ilivyo nzuri wakati tunapoteza maana ya muda kwa ajili ya kuwapatia umakini wale ambao tunakukutana nao, na ndivyo ilivyo. Yesu akijisahau hata kula, hata hivyo alimwilishwa na mapenzi ya Mungu ya kuwafikia wote katika kina. Ndivyo Msamamaria aligeuka kuwa wa kwanza kati ya wengi wainjilishaji. Kutoka kudharauliwa kwake katika kijiji, kwa aliyetengwa, wengi kwa ushuhuda wake, walikuja kukutana na Yesu, na hata kwao kwa imani inabubujika kama maji safi.
Kuhudumia ubinadamu ulio na kiu ya ukweli na haki
Kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu Leo XIV alisema kuwa "Kaka na dada, kwake Maria, Mama wa Kanisa, tuombe leo hii, ili kuweza kuhudumu na Yesu na kama Yesu, ubinadamu ulio na kiu ya ukweli na haki. Si wakati wa kupingana kati ya wakati na ‘mwingine’ na ‘wengine’, kati ‘yetu’ na ‘wengine’: waabuduo ambao Mungu anatafuta ni wanaume na wanawake wa amani ambao wanamwabudu katika Roho na Ukweli(Yh 4,23-24).
Asante kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here
