Papa Leo XIV:Usidharau kamwe ukatili dhidi ya wanawake,ripoti bila woga
Na Salvatore Cernuzio –Vatican.
Barua ya Papa Leo XIV, iliyochapishwa katika toleo la mwezi Machi katika jarida la "Piazza San Pietro" na kutolewa tarehe 8 Machi 2026, katika Siku ya Kimataifa ya Wanawake, ni heshima kwa wanawake, ambao mara nyingi "hupigwa na kuuawa" leo hii kwa sababu wao ni ishara ya utata katika jamii iliyochanganyikiwa na yenye vurugu. Pia ni wito mkubwa wa kuwaunga mkono na kuwalinda kwa kukemea na kutopuuza kila kitendo cha vurugu. Papa anajibu—kama kawaida—ombi la msomaji la msaada au chakula cha mawazo na hatua kuhusu masuala ya sasa.
Giovanna alisaini barua hiyo ya mwezi Machi ambaye anaandika kutokea Roma, "akiwa na machozi machoni pake," akizungumzia misiba ya wanawake wengi ambao kwa "kumpenda mwanamume, kumuoa, au kuchagua kuishi naye, kuanzisha familia" kunakuwa "mtego." "Kwa nini?" anauliza: "Tunawezaje kuelezea leo hii vurugu za mara kwa mara na zenye uchungu ambazo wanaume wengi hutumia dhidi ya wanawake wanaodai kuwapenda? Hadi kufikia hatua ya kuwaua kikatili, kwa chuki, kana kwamba walikuwa na hatia ya kutowapenda tena."
Kuunga mkono fikra ya kike
Jibu la Papa Leo XIV ni refu na la kufikiria, kuanzia hisia ya "mateso makubwa" ambayo suala hili linamsababisha: "Ukatili katika mahusiano, na hasa unyanyasaji dhidi ya wanawake." Papa Leo XIV anamtaja Mtakatifu Yohane Paulo II na usemi maarufu wa "fikra ya kike," fikra hiyo ambayo "katika ulimwengu ambao mara nyingi unatawaliwa na mawazo ya vurugu, unapaswa kuungwa mkono zaidi."
Ishara ya utata
Wanawake ni "wahusika wakuu na waundaji wa utamaduni wa utunzaji na udugu ambao ni muhimu kwa kutoa mustakabali na heshima kwa wanadamu wote," Papa Leo XIV anabainisha. "Labda hii pia ndiyo sababu" "wanapigwa na kuuawa" leo, anasisitiza, kwa sababu, "ni ishara ya utata katika jamii hii iliyochanganyikiwa, isiyo na uhakika, na yenye vurugu, kwa sababu wanatuelekeza kwenye maadili ya imani, uhuru, usawa, uzaaji, matumaini, mshikamano na haki." "Maadili haya makubwa," badala yake, "yanashambuliwa na mawazo hatari yanayoathiri mahusiano, na kutoa ubinafsi, ubaguzi na hamu ya kutawala."
Vurugu, mpaka unaotenganisha ustaarabu na ushenzi
Tayari katika mahubiri yake ya Pentekoste mnamo tarehe 8 Juni 2025 , pia katika hafla ya Jubilei ya Harakati , Papa Leo XIV alilaani mtazamo huu, ambao "mara nyingi husababisha vurugu, kama visa vingi vya hivi karibuni vya mauaji ya wanawake vinavyoonesha kwa huzuni." "Vurugu, vurugu yoyote, ndio mpaka unaotenganisha ustaarabu na ushenzi," Papa alisisitiza. "Hatupaswi kamwe kudharau kitendo cha vurugu, na hatupaswi kuogopa kukemea vurugu, ikiwa ni pamoja na hali ya kuhesabiwa haki au ambayo hupunguza au kukataa uwajibikaji."
Muungano wa Shule na Kanisa
Kisha Papa Leo XIV alielezea shukrani zake za dhati kwa wito wa Giovanna wa kazi ya "mahalia" kuhusu utamaduni na elimu ya vijana ili "kusaidia kukuza heshima kwa jinsia tofauti na kwa wengine, kwa maana pana zaidi kwa wale walio tofauti nasi." Na hii ni kazi, kulingana na msomaji wa Roma wa jarida lililohaririwa na Padre Enzo Fortunato, ambayo, Shule na Kanisa zinaweza kufanya kwa pamoja: "Ni nani mwingine kama siyo Shule na Kanisa vinaweza kusaidia vizazi vipya kwa kueneza utamaduni wa heshima, upendo, na zaidi ya yote, uhuru? Ujumbe unaotufundisha kutowachukulia wanawake kama vitu vya kumilikiwa..."
Mipango Maalum
Kwa hivyo, Giovanna anatoa wito wa "muungano wenye nguvu zaidi wa kielimu," na Papa Leo anasisitiza umuhimu wake kamili: "Kutembea pamoja kwa heshima ya pande zote kwa ubinadamu wetu si ndoto, bali ni ukweli pekee unaowezekana wa kujenga ulimwengu wa nuru kwa wote," anaandika katika barua hiyo. "Kanisa, pamoja na familia, shule, parokia, harakati na vyama vya kitume, mashirika ya kitawa na taasisi za umma zinaweza kushiriki hitaji la dharura la kutekeleza mipango maalum ya kuzuia na kukomesha ukatili dhidi ya wanawake," anaadika.
Kuwaelimisha Vijana
Kuanzia hapa, ndivpo unakuja wito mwingine wa kufuatia ule uliotolewa manmo tarehe 25 Novemba 2025, wakati wa Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake “kukomesha ukatili” kuanzia na “elimu ya vijana” na kutafuta kufungua “moyo wa kila mtu kusema kwamba kila mtu ni mwanadamu anayestahili heshima, heshima hiyo kwa wanaume na wanawake, kwa kila mtu.” “Lazima tuondoe ukatili huu, na kutafuta njia za kuunda mawazo ya watu; lazima tuwe watu wa amani, wanaowapenda kila mtu," alihitimisha Papa.
Asante kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here
