Papa Leo XIV ameondoka kwenda Ufalme wa Monaco
Vatican News
Ikuwa saa 1.22 asubuhi, majira ya Ulaya, Jumamosi tarehe 28 Machi 2026, ambapo Helikopta akiwemo Baba Mtakatifu Leo XIV iliondoka kwenye Kiwanja(Heliport)cha Helikopta cha Vatican. Papa anaelekea katika Ufalme wa Monaco, ambapo atafanya ziara yake ya Pili ya Kitume ya Kimataifa, ya kwanza na Papa katika nyakati za kisasa. Papa Leo anatarajiwa kutua saa 3:00 asubuhi katika Jiji la Serikali ndogo, ambapo Ukatoliki ndiyo dini rasmi na ambapo Papa atabaki kwa chini ya masaa tisa.
Wakati akiondoka nchini Italia, Papa Leo XIV alituma telegramu ya kiutamaduni kwa Rais wa Jamhuri ya Italia, Bwana Sergio Mattarella, akielezea kwamba anaondoka kwenda Monaco "akitamani kuhimiza ushuhuda wao wa Kikristo na ujenzi wa manufaa ya wote." Kwa Mkuu wa Serikali ya Italia kwa njia hiyo alitoa "salamu za dhati," pamoja na "matashi ya dhati kwa maendeleo ya kiroho, kiraia, na kijamii ya taifa la Italia."
Katika siku hii, matukio manne makuu yataashiria Ziara ya kitume: ziara ya heshima kwa Mfalme Albert katika Jumba la Kifalme, mkutano na jumuiya ya Wakatoliki katika Kanisa Kuu la Mama Yetu Asiye na dhambi ya Asili na mkutano na vijana na wakatekumeni katika Uwanja ulio mbele ya Kanisa Mtakatifu Devota.
Hatimaye, Misa ya mwisho itafanyika katika Uwanja wa Mchezo wa Louis II. Karibu musa wa saa 11:45 jioni, Baba Mtakatifu Leo XIV anatarajia kuondoka Monaco kwa Helikopta tena kurudi Vatican.
Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican alizungumzia matarajio ya ziara hii katika mahojiano na vyombo vya habari vya Vatican, huku akielezea matumaini kwamba "safari hii itatoa msukumo mpya kwa utume wa Kanisa mahalia, ikiimarisha ahadi yetu ya pamoja katika nyanja za dharura" kama vile ulinzi wa uumbaji, ulinzi wa maisha, na kukuza mshikamano wa kimataifa, bila kusahau "walio hatarini zaidi."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.
