Papa Leo XIV alikutana na Urais Bosnia na Herzegovina
Vatican News
Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana na Rais wa zamu wa Urais wa pamoja wa Bosnia na Erzegovina, Bwana Željko Komšić, Mwenyekiti wa Zamu Bwana Denis Bećirović na Bi Željka Cvijanović, ambao baada ya mkutano huo walikutana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Nchi na Mashirika ya Kimataifa.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Habari ya Vatican imebainisha kuwa "Wakati wa mazungumzo yao ya kirafiki katika Sekretarieti ya Vatican shukrani zilitolewa kwa uhusiano mzuri wa pande mbili. Umakini ulitolewa kwa hitaji la mazungumzo jumuishi na yenye kujenga ili kuhakikisha utulivu wa nchi na usawa wa kisheria na kijamii wa watu wake wote."
Hatimaye, "masuala kadhaa ya kikanda na kimataifa yalishughulikiwa, kama vile amani na usalama katika Balkani Magharibi na athari za migogoro inayoendelea nchini Ukraine na Mashariki ya Kati."
Asante kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here.
