2026.03.08 Papa  Leo XIV akutana na Bwana Zeljko Komsic,Rais wa Zamu wa Urais wa Pamoja wa Bosnia na  Erzegovina. 2026.03.08 Papa Leo XIV akutana na Bwana Zeljko Komsic,Rais wa Zamu wa Urais wa Pamoja wa Bosnia na Erzegovina.  (@VATICAN MEDIA)

Papa Leo XIV alikutana na Urais Bosnia na Herzegovina

Papa Leo XIV Jumatatu Machi 9 alikutana katika katika Jumba la Kitume la Vatican, na Rais wa Zamu wa Urais wa Pamoja wa Bosnia na Erzegovina, ikifuatiwa na majadiliano katika Sekretarieti ya Vatican. Miongoni mwa mada zilizojadiliwa ni amani na usalama katika Nchi za Balkani za Magharibi na athari za migogoro inayoendelea nchini Ukraine na Mashariki ya Kati.

Vatican News

Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana na Rais wa zamu wa Urais wa pamoja wa Bosnia na Erzegovina,  Bwana Željko Komšić, Mwenyekiti wa Zamu Bwana Denis Bećirović na Bi  Željka Cvijanović, ambao baada ya mkutano huo walikutana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Nchi na Mashirika ya Kimataifa.

Papa Leo XIV na viongozi wa Bosnia na Erzegovina
Papa Leo XIV na viongozi wa Bosnia na Erzegovina   (@VATICAN MEDIA)

Kwa mujibu wa Ofisi ya Habari ya Vatican imebainisha kuwa "Wakati wa mazungumzo yao ya kirafiki katika Sekretarieti ya Vatican shukrani zilitolewa kwa uhusiano mzuri wa pande mbili. Umakini ulitolewa  kwa hitaji la mazungumzo jumuishi na yenye kujenga ili kuhakikisha utulivu wa nchi na usawa wa kisheria na kijamii wa watu wake wote."

Kubadilishana zawadi
Kubadilishana zawadi   (@VATICAN MEDIA)

Hatimaye, "masuala kadhaa ya kikanda na kimataifa yalishughulikiwa, kama vile amani na usalama katika Balkani Magharibi na athari za migogoro inayoendelea nchini Ukraine na Mashariki ya Kati."

Asante kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here.

09 Machi 2026, 12:42