Papa Leo XIV akutana na Waziri Mkuu wa Bosnia na Herzegovina
Vatican News
Papa Leo XIV, tarehe 26 Machi 2026, alimpokea Borjana Krišto, Waziri Mkuu wa Bosnia na Herzegovina, ambaye baadaye alikutana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.
Mazungumzo katika Sekretarieti ya Vatican
"Wakati wa majadiliano ya kirafiki katika Sekretarieti ya Vatican, kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Habari ya Vatican ilibanisha, "kuthaminiana kwa uhusiano mzuri wa pande mbili na mchango wa Kanisa mahalia kwa jamii kulithibitishwa tena. Katika muktadha huo, umakini maalum ulitolewa kwa hali ya Jumuiya Wakatoliki na masuala mengine muhimu katika uhusiano wa Kanisa na Serikali." "Wakati wa majadiliano," taarifa inaendelea, "kulikuwa na kubadilishana maoni kuhusu upanuzi wa Umoja wa Ulaya kwa nchi za Balkan Magharibi."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.
