2026.03.26 Bi Borjana Kristo, Waziri Mkuu wa Bosnia na Erzegovina 2026.03.26 Bi Borjana Kristo, Waziri Mkuu wa Bosnia na Erzegovina  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV akutana na Waziri Mkuu wa Bosnia na Herzegovina

Baba Mtakatifu alikutana na Bi Borjana Krišto,Waziri Mkuu wa Bosnia na Herzegovina,katika Jumba la Kitume la Vatican.Wakati wa majadiliano yao katika Sekretarieti ya Vatican ambapo walijikita na masuala muhimu katika uhusiano wa Kanisa na Serikali na kubadilishana mawazo kuhusu upanuzi wa Umoja wa Ulaya hadi Balkani za Magharibi.

Vatican News

Papa Leo XIV, tarehe 26 Machi 2026, alimpokea Borjana Krišto, Waziri Mkuu wa Bosnia na Herzegovina, ambaye baadaye alikutana na Askofu Mkuu  Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.

Mazungumzo katika Sekretarieti ya Vatican

"Wakati wa majadiliano ya kirafiki katika Sekretarieti ya Vatican, kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Habari ya Vatican ilibanisha, "kuthaminiana kwa uhusiano mzuri wa pande mbili na mchango wa Kanisa mahalia kwa jamii kulithibitishwa tena. Katika muktadha huo, umakini maalum ulitolewa kwa hali ya Jumuiya  Wakatoliki na masuala mengine muhimu katika uhusiano wa Kanisa na Serikali." "Wakati wa majadiliano," taarifa inaendelea, "kulikuwa na kubadilishana maoni kuhusu upanuzi wa Umoja wa Ulaya kwa nchi za Balkan Magharibi."

PAPA NA WAZIRI MKUU WA BOSNIA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

26 Machi 2026, 16:20