Papa Leo XIV amkumbuka Kardinali Pham Minh Mân:"Mhamasishaji wa umoja"
Vatican News
Baba Mtakatifu Leo XIV ameelezea "huzuni" yake kuhusu kifo cha Kardinali wa Vietnam Jean-Baptiste Pham Minh Mân, aliyekuwa Askofu Mkuu Mstaafu wa Jiji la Than-Phô Ho Chi Minh, ambaye alifariki Dominika tarehe 22 Machi 2026, juma chache baada ya kutimiza miaka 92, tarehe 5 Mahi 2026. Katika telegramu iliyotolewa tarehe 26 Machi 2026 ilikielekezwa kwa Askofu Mkuu Joseph Nguyễn Năng, wa Jiji la Ho Chi Minh, Papa alielezea rambirambi zake "kwa mapadre, watawa, na waamini walei wa jimbo kuu" na anakumbuka "kwa shukrani kubwa miaka yake mingi ya huduma ya kikuhani na kiaskofu katika makanisa ya ndani ya Jiji la My Tho na Ho Chi Minh, pamoja na michango yake kwa Kanisa huko Vietnam na kwa Vatican.
Maisha aliyoishi kwa unyenyekevu
Papa Leo XIV alisisitiza zaidi kujitolea kwa Kardinali kwa "utunzaji wa kichungaji," ushiriki wa kijamii, na "kukuza mazungumzo na umoja wa kikanisa kila mara." Katika maandishi yake, Baba Mtakatifu aliakisi "ushuhuda wa maisha aliyoishi kwa urahisi na unyenyekevu wa kiinjili." Hatimaye, alitoa baraka zake "kama ishara ya faraja na amani katika Bwana" kwa wale wanaoomboleza kifo cha Kardinali Jean-Baptiste Pham Minh Mân, "katika tumaini la uhakika la Ufufuo."
Huduma yake ndefu ya kichungaji
Mazishi ya Kardinali yatafanyika Ijumaa tarehe 27 Machi 2026 , saa 2.30 asubuhi katika Kituo cha Kichungaji cha Jimbo Kuu la Hôchiminh Ville. Baada ya kuwa Padre akiwa na umri wa miaka 31, mnamo 1965, aliteuliwa kuwa Askofu Mwandamizi wa My Tho, mwenye haki ya urithi, na akapewa daraja la uaskofu mnamo tarehe 11 Agosti 1993. Kuanzia 2001 hadi 2007, alihudumu kama Makamu Rais wa Baraza la Maaskofu wa Vietnam. Katika Mkutano wa tarehe 21 Oktoba 2003, aliumbwa na kutangazwa kuwa Kardinali na Mtakatifu Yohane Paulo II, kwa kuwa na Kanisa la Roma la Mtakatifu Justin.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.
