Kardinali wa Vietnamu Jean-Baptist Pham Minh Mân ameaga dunia
Vatican News
Kardinali Jean-Baptist Pham Minh Mân, Askofu Mkuu Mstaafu wa Thàn-Phô Hô Chí Minh, Jiji la Hochiminh, aliaga dunia Dominika tarehe 22 Machi 2026, katika Kituo cha Kichungaji cha Jimbo Kuu huko Viêt Nam, majuma kadhaa baada ya kutimiza umri wa miaka 92. Hioni ya Dominika hiyo, Parokia zote katika Jiji la Hochiminh zilipiga kengele zao kwa huzuni. Alizaliwa Ca Mau, katika Jimbo Can Tho, mnamo tarehe 5 Machi 1934, na akawekwa daraja la Upadre mnamo tarehe 25 Mei 1965.
Mnamo tarehe 22 Machi 1993, aliteuliwa kuwa Askofu Mwandamizi wa My Tho mwenye haki ya urithi, na alipewa Wakfu wa Kiaskofu mnamo tarehe 11 Agosti 1993. Mnamo tarehe 1 Machi 1998, alipandishwa wadhifa hadi Kiti cha Metropolitan, yaani kuwa Askofu Mkuu wa Than-Phô Ho Chi Minh. Kuanzia 2001 hadi 2007, alihudumu kama Makamu Rais wa Baraza la Maaskofu wa Vietnam.
Katika kikao cha tarehe 21 Oktoba 2003, aliundwa na kutangazwa kuwa Kardinali na Mtakatifu Yohane Paulo II, akiwa na kiti cha Kanisa la Mtakatifu Giustino.
Mnamo tarehe 22 Machi 2014, alijiuzulu kutoka kutoka shughuli za kichungaji wa Than-Phô Ho Chi Minh baada ya kutimiza miaka yake ya huduma. Mazishi yake yataadhimishwa Ijumaa tarehe 27 Machi 2026, saa 2:30 asubuhi katika Kituo cha Kichungaji cha Jimbo Kuu.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.