Tafuta

Papa akutana na Mfalme na Malkia wa Hispania

Ijumaa Machi 20,Baba Mtakatifu alikutana na Mfalme Felipe VI, akifuatana na Malkia Letizia wa Hispania.Majadiliano yalifuata katika Sekretarieti ya Vatican,ambapo walirejea juu Ziara ya Kitume ijayo ya Papa katika nchi hiyo na umuhimu wa kujitolea kuendelea kwa amani.

Vatican News

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya habari vya Kiti Kitakatifu, Ijumaa  asubuhi tarehe 20 Machi 2026, Baba Mtakatifu Leo XIV aliwapokea Mfalme Felipe VI na Malkia Letizia wa Hispania katika Jumba la Kitume mjini Vatican. Baadaye, familia ya kifalme ilikutana na Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa  Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.

Mkutano huo ulilenga "uhusiano mzuri kati ya Kiti Kitakatifu na Hispania, ambao utakuwa na matokeo yake makubwa, kwa mujibu wa taarifa hiyo inavyosomeka, "katika Ziara  ya Kitume ya Baba Mtakatifu ijayo." Pia walijadili masuala kadhaa ya sasa kuhusu hali ya nchi na Utume wa Kanisa katika jamii.

Wakati wa kubadilishana zawadi na wafalme wa Hispania

Miongoni mwa mada zilizojadiliwa pia ni umuhimu wa kujitolea mara kwa mara katika kuunga mkono amani" na uimarishaji wa kanuni na maadili yanayounga mkono kuishi pamoja kimataifa.

I Reali di Spagna insieme al cardinale Pietro Parolin

Wafalme wa Hispania wakiwa na Kardinali Pietro Parolin   (@Vatican Media)

Katika kubadilishana zawadi na Papa, Mfalme Felipe na Malkia Letizia waliwasilisha Kitabu cha Saa cha Philip II cha karne ya 16. Ni kazi ya kipekee zaidi iliyoundwa katika  Monasteri ya Kifalme ya El Escorial, ambapo imehifadhiwa.

Wafalme wa Hispania wakisindikizwa

Baada ya kuondoka mjini Vatican, familia ya kifalme ilihamia katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu(Santa Maria Maggiore), ili Mfalme Filipe wa VI kupokea jina la Mkanoni wa Kanisa Kuu la Kipapa.

PAPA NA WAFALME

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.

20 Machi 2026, 13:41