Papa akutana na Mfalme na Malkia wa Hispania
Vatican News
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya habari vya Kiti Kitakatifu, Ijumaa asubuhi tarehe 20 Machi 2026, Baba Mtakatifu Leo XIV aliwapokea Mfalme Felipe VI na Malkia Letizia wa Hispania katika Jumba la Kitume mjini Vatican. Baadaye, familia ya kifalme ilikutana na Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.
Mkutano huo ulilenga "uhusiano mzuri kati ya Kiti Kitakatifu na Hispania, ambao utakuwa na matokeo yake makubwa, kwa mujibu wa taarifa hiyo inavyosomeka, "katika Ziara ya Kitume ya Baba Mtakatifu ijayo." Pia walijadili masuala kadhaa ya sasa kuhusu hali ya nchi na Utume wa Kanisa katika jamii.
![]()
Wakati wa kubadilishana zawadi na wafalme wa Hispania
Miongoni mwa mada zilizojadiliwa pia ni umuhimu wa kujitolea mara kwa mara katika kuunga mkono amani" na uimarishaji wa kanuni na maadili yanayounga mkono kuishi pamoja kimataifa.
![]()
Wafalme wa Hispania wakiwa na Kardinali Pietro Parolin (@Vatican Media)
Katika kubadilishana zawadi na Papa, Mfalme Felipe na Malkia Letizia waliwasilisha Kitabu cha Saa cha Philip II cha karne ya 16. Ni kazi ya kipekee zaidi iliyoundwa katika Monasteri ya Kifalme ya El Escorial, ambapo imehifadhiwa.
Wafalme wa Hispania wakisindikizwa
Baada ya kuondoka mjini Vatican, familia ya kifalme ilihamia katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu(Santa Maria Maggiore), ili Mfalme Filipe wa VI kupokea jina la Mkanoni wa Kanisa Kuu la Kipapa.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.
