Tafuta

2026.02.14 S.E. Papa na Bwana Josà Ulisses Correia na  Silva, Waziri Mkuu wa Primo Cabo Verde 2026.02.14 S.E. Papa na Bwana Josà Ulisses Correia na Silva, Waziri Mkuu wa Primo Cabo Verde   (@VATICAN MEDIA)

Papa Leo XIV akutana na Waziri Mkuu wa Cabo Verde

Katika Jumba la Kitume,Papa alimpokea na kuzungumza na Waziri Mkuu José Ulisses Correia na Silva.Na katika Sekretarieti ya Vatican,majadiliano pia yalilenga usalama katika eneo la Afrika Magharibi.

Vatican News

Jumamosi tarehe 14  Februari 2026, Baba. Mtakatifu Leo XIV  alimpokea na kuzungumza na José Ulisses Correia na Silva, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Cabo Verde, katika Jumba la kitume, Vatican. Hii iliripotiwa katika taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Vatican.

Papa na Waziri Mkuu wa Cabo Verde
Papa na Waziri Mkuu wa Cabo Verde   (@VATICAN MEDIA)

Mwishoni mwa mkutano huo, Waziri Mkuu huyo alikutana na Kardinali Pietro Parolin, akifuatana na Monsinyo Mihăiţă Blaj, Katibu Msaidizi wa  Vatican wa Mahusiano na Mashirika ya Kimataifa.

Picha ya pamoja na wasindikizaji wake
Picha ya pamoja na wasindikizaji wake   (@VATICAN MEDIA)

"Wakati wa majadiliano ya kirafiki," maandishi yanasema, "hali chanya ya uhusiano kati ya Vatican na Jamhuri ya Cabo Verde ilithibitishwa tena, hasa ikimaanisha mchango wa Kanisa Katoliki nchini humo na utekelezaji wa makubaliano ya pande mbili yaliyoidhinishwa mwaka  2014."

Katibu Mkuu wa Vatican na Waziri Mkuu wa Cabo Verde
Katibu Mkuu wa Vatican na Waziri Mkuu wa Cabo Verde   (@Vatican Media)

Mkutano huo pia ulizungumzia baadhi ya vipengele vya hali ya kijamii na kiuchumi kitaifa. Pia walibadilishana maoni kuhusu masuala ya sasa ya kikanda, hasa masuala ya usalama katika eneo la Afrika Magharibi.

Mazungumzo katika Sekretarieti ya Vatican
Mazungumzo katika Sekretarieti ya Vatican   (@Vatican Media)

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

 

14 Februari 2026, 15:59