Tafuta

2026.02.13 Papa kwa Vikosi vya Polisi Kampuni ya Roma- Mtakatifu Petro. 2026.02.13 Papa kwa Vikosi vya Polisi Kampuni ya Roma- Mtakatifu Petro.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV kwa Polisi:gundueni upya ujumbe wa Kikristo&mfanye kazi kwa dhamiri njema!

Akihutubia vikosi vya Polisi vya Roma-Jumuiya ya Mtakatifu Petro,Papa Leo XIV alibainisha kwamba ujumbe wa Yesu umeenea katika miundo na njia za kutenda kupitia"mapinduzi"yasiyo na vurugu kwa karne nyingi:"Je,hili silo linaloweza na lazima litokee katika kila kizazi,hata ulimwenguni na Roma leo hii?"Amewasihi waishi uongozi hai na utii katika nuru ya Injili.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Uongozi, amri, utii, uzoefu wenye changamoto lakini wenye utajiri wa Jubilei, jijini Roma, kutangazwa kwa habari Njema, mapinduzi yasiyo na vurugu ya Injili, kugundua upya asili muhimu ya ujumbe wa Kikristo na  kufanya kazi kwa dhamiri njema, ni maneno yaliyomo kwenye hotuba ya Baba Mtakatifu Leo XIV alipokutana na Vikosi vya Polisi, Roma -Jumuiya ya Mtakatifu Petro, Ijumaa tarehe 13 Februari 2026, katika Ukumbi wa Clementine wa Jumba la Kitume la Vatican. Miongoi mwa walioudhuria mkutano ni pamoja na Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Polisi Salvatore Luongo.

Papa akihutubia vikosi vya Polisi
Papa akihutubia vikosi vya Polisi   (@Vatican Media)

Papa alifurahishwa na majibu aliyopokea kutoka kwa wanachama wa Polisi wakati wa Jubilei iliyomalizika hivi karibuni: kwani alisema kuwa ulikuwa uzoefu "wenye changamoto kubwa" lakini pia "unaotajirisha", kibinadamu na kitaaluma. “Namshukuru Bwana kwa hili. Hakika, hii imekuwa hivyo kwetu sote tunaoishi Roma: ushuhuda wa mahujaji wengi umetujenga.” Kuanzia nyakati za hivi karibuni hadi mwanzo wa Ukristo, Papa alikumbuka jinsi jijini Roma, katika vitengo vyake mbalimbali, ikiwa ni pamoja na ile ya kijeshi, "Habari Njema" ya Yesu ilianza kuenea mapema: njia mpya ya kuishi na kufikiri, iliyoongozwa na Mungu ambaye amekuwa upendo, huruma, na msamaha,” Papa alisisitiza.

Picha ya Pamoja
Picha ya Pamoja   (@VATICAN MEDIA)

Udugu miongoni mwa wanaume na wanawake wote unaopita tofauti zote za kijamii na kikabila, alisistiza. Miundo ya shirika, pamoja na utumiaji wa mamlaka na nidhamu, ni ya kawaida katika mfumo wa uendeshaji wa kijeshi na, ikiwa itatafsiriwa upya kwa nuru ya Injili, pia kwa ule wa Kanisa. Hakika, kwa karne nyingi, Baba Mtakatifu Leo XIV aliendelea, ujumbe wa Yesu umepenya miundo, vigezo, njia za kutenda na kufikiri kwa  ustaarabu mwingi. Haukufanya hivyo kupitia mapinduzi ya vurugu, bali kupitia mabadiliko ya amani, kutoka ndani, kupitia dhamiri, ubadilishaji wa mioyo. Kwa njia hiyo, Injili inaeneza "hisia ya Mungu na mwanadamu," ikithibitisha tena heshima "kamili" kwa kuwepo na utu wa mwanadamu, "pamoja na ibada ya Mungu na Yeye pekee."

Polisi wa -Roma na Jumuiya ya Mtakatifu Petro
Polisi wa -Roma na Jumuiya ya Mtakatifu Petro   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu Leo aidha aliuliza  kama  hili silo hasa "linaloweza na lazima litokee katika kila kizazi, hata Ulimwenguni na Roma leo hii." Jibu la kuthibitisha linalopata msingi wake katika ngazi ya "juu" ya Majisterio ya kikanisa, ni  Mtaguso wa Pili wa Vatican. Tumeitwa kugundua upya kiini cha ujumbe wa Kikristo na mtindo wa Kanisa changa, ili kuvifanya viwe mwili katika ulimwengu wetu tofauti sana na mgumu zaidi. Lakini Yesu Kristo ni yule yule jana, leo, na hata milele,” Papa alibainisha. Kwa kuhitimisha Papa Leo XIV aliwashukuru Polisi kwa huduma yao, hasa katika eneo la Vatican  na jiji la Roma. Ni matumaini yake kwamba kila mmoja wao atimize wajibu wake kwa "dhamiri safi," waaminifu kwa kanuni za Kipolisi, na  kama Wakristo, wawe waaminifu kwa Injili, "ambayo inajaza kila nia na kila tendo kwa upendo wa Kristo."

PAPA LEO NA POLISI

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

13 Februari 2026, 12:30