Papa Leo XIV katika Groto ya Lourdes:Maria anatufudisha maana ya mateso na upendo
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mara baada ya Katekesi yake kwenye ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican, Jumatano tarehe 11 Februari 2026, kama alivyokuwa ameeleza waamini na mahujaji, Baba Mtakatifu alikwenda katika Groto ya Lourdes iliyopo katika Bustani za Vatican katika Siku ya Wagonjwa Duniani sanjari na Siku Kuu ya Bikira Maria wa Lourdes.
Hapo aliwakuta baadhi ya wagonjwa ambapo aliwasha mshamaa na kusali pamoja nao. Papa Leo alisema“Leo, katika siku hii iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa, tunataka kuomba kwa ushirika na wale wote wanaoteseka ulimwenguni kote. Tunao kwa ajili yenu. Ninakushukuru kwa dhati kwa kufanya juhudi za kufika na kusindikizana nasi katika wakati huu wa maombi, hapa mbele ya mama yetu, Maria, kwenye ukumbusho wake wa kiliturujia, Mama Yetu wa Lourdes.”
“Ni siku nzuri sana inayotukumbusha ukaribu wa Maria, mama yetu, ambaye husindikizana nasi kila wakati na kutufundisha mengi: Maana ya mateso, upendo, na kusalimisha maisha ya mtu mikononi mwa Bwana.”
“Kwa hivyo, tunaomba pia baraka za Bwana kwa ajili yenu, kwa wagonjwa wote leo na siku zote, na kwa wale wote wanaowasindikiza: sayansi ya matibabu, madaktari, wauguzi, watu wengi walio karibu nasi, hasa katika nyakati ngumu zaidi. Tuombe pamoja: Salamu Maria...
Baraka. … Asante Mungu awasindikize daima.”
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here.
