Papa Leo XIV atoa heshima kwa Mama wa Lourdes katika Siku ya Wagonjwa Duniani
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Watakatifu Cyril na Methodius, mitume wa Kslavi na walinzi wa Ulaya, wanaweza kusaidia kuifufua Ulaya, ndilo lilikuwa wazo la Papa Leo XIV, ambaye, katika salamu zake kwa mahujaji wa Poland waliokuwepo katika Katekesi yake aliwakumbuka "mababa wa Ukristo, lugha na utamaduni wa watu wa Kislavi. Kiukweli ukumbusho wao wa kiliturujia utaadhimishwa tarehe 14 Februari 2026.
"Turudi kwenye kazi yao ya kitume, kama Mtakatifu Yohane Paulo II alivyohimiza katika kujenga umoja mpya katika bara la Ulaya, ili kushinda mivutano, migawanyiko na uadui wa kidini na kisiasa," Papa alisema.
Ombi kwa Wagonjwa
Hata hivyo wito wa umoja wa Ulaya umekuja katika Siku ya Wagonjwa Duniani. Ili kuisherehekea siku hii, Papa Leo XIV katika Ukumbi wa Paulo VI, aliwasha mshumaa mbele ya sanamu ya Bikira Maria wa Lourdes, katika siku ambayo Mama Kanisa anaadhimisha kumbukumbu yake, huku kila mtu akiimba wimbo wa Ave Maria yaani Salamu Maria wa Lourdes, na kisha Papa Leo alieleza ambavyo angekwenda kusali kwenye Bustani za Vatican, mahali ambapo kuna Groto ya Mama wa Lourdes:
"nitakwenda kwenye Pango la Lourdes katika Bustani za Vatican na kuwasha mshumaa, ishara ya sala yangu kwa wagonjwa wote, ambao tunawakumbuka kwa upendo maalum leo hii katika Siku ya Wagonjwa Duniani," alifafanua Papa.
Wito wa mshikamano kwa Colombia
Kwa lugha ya Kihispania, alikumbusha kwamba maadhimisho ya mwaka huu yanaadhimishwa katika Mahali Patakatifu pa Mama Yetu wa Amani huko Chiclayo, mahali ambapo Baba Mtakatifu aliungana nao kiroho. Na alimtuma Kardinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu, kwenda Peru kama mwakilishi wake katika Siku hii ya Wagonjwa Duniani.Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu aliwakabidhi wagonjwa na familia zao kwa Maria.
Papa alisema: “Pia ninawakabidhi ulinzi wake waathirika wote walioathiriwa na mafuriko makubwa huko Colombia, huku nikihimiza jamii nzima kuunga mkono familia zilizoathiriwa kwa upendo na sala.”
Kwa Mama Yetu wa Lourdes, katika ukumbusho wa kiliturujia, Papa Leo XIV, katika salamu yake kwa lugha ya Kiitaliano, aliwakabidhi vijana, wagonjwa, na wenye ndoa wapya ili aweze "kuwaombea mbele za Mungu na kuwapatia neema za kuwategemeza katika safari yenu."
Kwaresima, ni kipindi cha Maombi
"Jumatano ijayo ni mwanzo wa Kwaresima:” Papa alisema hayo, kwa lugha ya Kiingereza, akifafanua kipindi hiki kama muhimu: "kuongeza maarifa yetu na upendo wetu kwa Bwana, kuchunguza mioyo yetu na maisha yetu, na kuelekeza mitazamo yetu kwa Yesu na upendo wake kwetu." Siku hizi za maombi, kufunga, na kutoa sadaka ziwe chanzo cha nguvu tunapojitahidi kila siku kuchukua msalaba wetu na kumfuata Kristo.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here.
