Tafuta

2026.01.17  Mfalme  Albert II wa Monaco na Papa Leo XIV. 2026.01.17 Mfalme Albert II wa Monaco na Papa Leo XIV.  (@VATICAN MEDIA)

Papa akutana na Mfalme Albert II wa Monaco

Baba Mtakatifu Leo Leo XIV,Jumamosi Januari 17 katika Jumba la Kitume la Vatican alikutana na Mfalme wa Momaco na baadaye yalifuata majadiliano katika Sekretarieti ya Vatican.Mahusiano mazuri ya pande mbili yaliyopo yalisisitizwa,kwa kurejea mchango wa kihistoria na muhimu wa Kanisa Katoliki katika maisha ya kijamii ya Kifalme.

Vatican News

Jumamosi tarehe 17 Januari 2026, Baba Mtakatu Leo XIV alimpokea Mfalme  Albert II wa Monaco katika Mkutano wao katika Jumba la Kitume la Vatican. Baadaye Mfalme huyo alikutana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.

Majadiliano kuhusu mazingira, misaada ya kibinadamu, na ulinzi wa utu wa binadamu

Kutoka taarifa za Ofisi ya Habari ya Kiti Kitakatifu inasema "Wakati wa majadiliano ya kirafiki katika Sekretarieti ya Vatican, uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi mbili ulisisitizwa na kutajwa kwa mchango wa kihistoria na muhimu wa Kanisa Katoliki katika maisha ya kijamii ya Ufalme huo.

Mazungumzo yaliendelea, yakizingatia masuala kadhaa ya maslahi ya pamoja, kama vile ulinzi wa mazingira, misaada ya kibinadamu, na ulinzi na ukuzaji wa utu wa mwanadamu. Hatimaye," taarifa hiyo inahitimisha,pia kulikuwa na ubadilishanaji wa maoni kuhusu masuala ya kimataifa, hasa msisitizo kuhusu amani na usalama, na kuhusu hali ya jumla katika Mashariki ya Kati na katika baadhi ya maeneo ya Afrika.

Papa akutana na Mfalme wa Monaco

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

17 Januari 2026, 15:08