Papa akutana na Mfalme Albert II wa Monaco
Vatican News
Jumamosi tarehe 17 Januari 2026, Baba Mtakatu Leo XIV alimpokea Mfalme Albert II wa Monaco katika Mkutano wao katika Jumba la Kitume la Vatican. Baadaye Mfalme huyo alikutana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.
Majadiliano kuhusu mazingira, misaada ya kibinadamu, na ulinzi wa utu wa binadamu
Kutoka taarifa za Ofisi ya Habari ya Kiti Kitakatifu inasema "Wakati wa majadiliano ya kirafiki katika Sekretarieti ya Vatican, uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi mbili ulisisitizwa na kutajwa kwa mchango wa kihistoria na muhimu wa Kanisa Katoliki katika maisha ya kijamii ya Ufalme huo.
Mazungumzo yaliendelea, yakizingatia masuala kadhaa ya maslahi ya pamoja, kama vile ulinzi wa mazingira, misaada ya kibinadamu, na ulinzi na ukuzaji wa utu wa mwanadamu. Hatimaye," taarifa hiyo inahitimisha,pia kulikuwa na ubadilishanaji wa maoni kuhusu masuala ya kimataifa, hasa msisitizo kuhusu amani na usalama, na kuhusu hali ya jumla katika Mashariki ya Kati na katika baadhi ya maeneo ya Afrika.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here
