Tafuta

2025.09.29 Bwana  Umaro Sissoco Embalò,Rais wa Jamhuri ya Guinea Bissau. 2025.09.29 Bwana Umaro Sissoco Embalò,Rais wa Jamhuri ya Guinea Bissau.  (@VATICAN MEDIA)

Papa Leo XIV akutana na Rais wa Guinea Bissau,Bw.Embalò

Mara baada ya mkutano na Papa,Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau,Mheshimiwa Umaro Sissoco Embaló,alikutana na Kardinali Pietro Parolin,Katibu Mkuu wa Vatican akifuatana na Monsinyo Mirosław Wachowski.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV Jumatatu tarehe 29 Septemba 2025, alikutana katika Jumba la Kitume mjini Vatican, Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau, Mheshimiwa Umaro Sissoco Embaló. Baadaye alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican akifuatana na Monsinyo Mirosław Wachowski.

Mkutano wa Papa na Rais wa Bissau
Mkutano wa Papa na Rais wa Bissau   (@VATICAN MEDIA)
Wakati wa kubadilishana zawadi, Rais wa Bissau na Papa
Wakati wa kubadilishana zawadi, Rais wa Bissau na Papa   (@VATICAN MEDIA)

Wakati wa majadiliano ya dhati katika Sekretarieti ya Vatican, uhusiano mwema kati ya Vatican na Guinea-Bissau ulisisitizwa, kwa kukazia mchango wa Kanisa katika manufaa ya wote, hasa katika nyanja za elimu na afya. Baadaye katika mazungumzo hayo, watu hao wawili walikazia masuala fulani ya hali ya kisiasa, kijamii, na kiuchumi ya nchi hiyo na kubadilishana mawazo kuhusu mambo ya sasa ya kimataifa, Hayo yote yalitolewa na Ofisi ya Vyombo vya Habari, Vatican.

Ujumbe wa Guinea Bissau na Rais wake kwa picha ya pamoja na Papa
Ujumbe wa Guinea Bissau na Rais wake kwa picha ya pamoja na Papa   (@VATICAN MEDIA)
29 Septemba 2025, 16:00