Papa Leo XIV akutana na Rais wa Guinea Bissau,Bw.Embalò
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV Jumatatu tarehe 29 Septemba 2025, alikutana katika Jumba la Kitume mjini Vatican, Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau, Mheshimiwa Umaro Sissoco Embaló. Baadaye alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican akifuatana na Monsinyo Mirosław Wachowski.
Wakati wa majadiliano ya dhati katika Sekretarieti ya Vatican, uhusiano mwema kati ya Vatican na Guinea-Bissau ulisisitizwa, kwa kukazia mchango wa Kanisa katika manufaa ya wote, hasa katika nyanja za elimu na afya. Baadaye katika mazungumzo hayo, watu hao wawili walikazia masuala fulani ya hali ya kisiasa, kijamii, na kiuchumi ya nchi hiyo na kubadilishana mawazo kuhusu mambo ya sasa ya kimataifa, Hayo yote yalitolewa na Ofisi ya Vyombo vya Habari, Vatican.
