Papa akutana na Rais wa Honduras
Vatican News
Ijumaa tarehe 19 Septemba 2025, Baba Mtakatifu amekutana katika Jumba la Kitume mjini Vatican na Rais wa Jamhuri ya Honduras Iris Xiomara Castro Sarmiento.
![]()
Papa na Rais wa Honduras (@VATICAN MEDIA)
Baadaye, kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Habari ya Vatican, Mkuu wa Nchi alikutana na Katibu Mkuu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, akifuatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.
![]()
Papa na Rais wa Honduras Iris Xiomara Castro Sarmiento na wasindikizaji wake (@VATICAN MEDIA)
Wakati wa majadiliano katika Sekretarieti ya Vatican, marejeo yalifanywa kwa uhusiano mzuri kati ya Honduras na Kiti Kitakatifu, na jukumu la Kanisa na Vatican katika sekta ya kijamii, elimu, na utunzaji wa wahamiaji lilijadiliwa. Mada nyingine zenye maslahi kwa pande zote kuhusu hali ya sasa ya kijamii na kisiasa nchini na kanda pia zilijadiliwa.
![]()
Kubadilishana zawadi kama utamaduni(@VATICAN MEDIA)
