Papa Leo alikutana na Rais wa Jamhuri ya Honduras. Papa Leo alikutana na Rais wa Jamhuri ya Honduras.  (@VATICAN MEDIA)

Papa akutana na Rais wa Honduras

Baba Mtakatifu Leo XIV Septemba 19 alikutana na Bi Castro Sarmiento katika Jumba la Kitume Vatican.Baadaye amefanya mazungumzo na Sekretarieti ya Vatican kwa kujikita juu y anafasi ya Kanisa na Serikali katika muktadha wa kijamii,elimu na utunzaji wa wahamiaji.

Vatican News

Ijumaa tarehe 19 Septemba 2025, Baba Mtakatifu amekutana katika Jumba la Kitume mjini Vatican na Rais wa Jamhuri ya  Honduras Iris Xiomara Castro Sarmiento.

Il Papa e la presidente dell'Honduras

Papa na Rais wa Honduras   (@VATICAN MEDIA)

Baadaye, kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Habari ya Vatican, Mkuu wa Nchi alikutana na Katibu Mkuu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, akifuatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.

Il Papa con la presidente dell'Honduras Iris Xiomara Castro Sarmiento e il suo seguito

Papa na Rais wa Honduras Iris Xiomara Castro Sarmiento na wasindikizaji wake (@VATICAN MEDIA)

Wakati wa majadiliano katika Sekretarieti ya Vatican, marejeo yalifanywa kwa uhusiano mzuri kati ya Honduras na Kiti Kitakatifu, na jukumu la Kanisa na Vatican katika sekta ya kijamii, elimu, na utunzaji wa wahamiaji lilijadiliwa. Mada nyingine zenye maslahi kwa pande zote kuhusu hali ya sasa ya kijamii na kisiasa nchini na kanda pia zilijadiliwa.

Rais wa Honduras akisalimiana na Katibu Mkuu wa Vatican
Rais wa Honduras akisalimiana na Katibu Mkuu wa Vatican   (@VATICAN MEDIA)

Lo scambio dei doni

Kubadilishana zawadi kama utamaduni(@VATICAN MEDIA)

 

19 Septemba 2025, 18:35