Oktoba mosi,Papa Leo XIV atahutubia Mkutano wa Harakati ya Laudato si'
Vatican News
Katika Kituo cha Mariapolis cha Hatarakati ya Wafocolare huko Castel Gandolfo, Jumatano, Oktoba 1, "Mkutano wenye kauli mbiu “Kuinua Tumaini kwa Haki ya Tabianchi”utaanza. Mkutano huo wa kimataifa unaandaliwa na Harakati ya Laudato Si' kwa kushirikiana na washirika mbalimbali wa kikanisa na kitaasisi, utaadhimisha kumbukumbu ya miaka kumi ya Waraka wa Baba Mtakatifu Francisko kuhusu utunzaji wa uumbaji.
Tukio hilo lililopangwa hadi tarehe 3 Oktoba 2025 kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari, litawaleta pamoja zaidi ya viongozi 400 wa kidini, wataalamu wa tabianchi, wawakilishi wa mashirika ya kiraia na taasisi mbalimbali duniani, kwa lengo la kupanga hatua zinazofuata katika kutekeleza uongofu wa kiikolojia kwa kuzingatia mafundisho ya Kanisa. Papa Leo XIV ataongoza "Sherehe ya Matumaini" Jumatano alasiri.
Kikao hicho kitakuwa na shuhuda mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Waziri wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi wa Brazili, Marina Silva, na Gavana wa zamani wa California Arnold Schwarzenegger, ambaye kwa muda mrefu amekuwa akijitolea kwa mipango kuhusu ulinzi wa viumbe. Baada ya hotuba ya Papa, kutakuwa na wakati wa ishara na kiroho wa kujitolea kwa pamoja, ikifuatiwa na mkutano na kikundi cha washiriki wa mkutano. Siku zitakazofuata, Oktoba 2 na 3, zitakuwa na vipindi vya kufanya kazi, meza za pande zote, na nyakati za kiroho.
