Papa Leo XIV Papa Leo XIV  (@Vatican Media)

Oktoba mosi,Papa Leo XIV atahutubia Mkutano wa Harakati ya Laudato si'

Katika Mwaka wa kumi wa Waraka wa Papa Francisko,Papa Leo XIV atashiriki tukio la Kimataifa lenye kauli mbiu:Kuinua Tumaini kwa ajili ya Haki ya Tabianchi,”kwa kuwaona washiriki 400 kutoka viongozi wa kidini,wataalamu wa tabianchi wawakilishi wa kiraia na kitaasisi kutoka Ulimwenguni kote.

Vatican News

Katika Kituo cha Mariapolis cha Hatarakati ya Wafocolare huko Castel Gandolfo, Jumatano, Oktoba 1, "Mkutano wenye kauli mbiu “Kuinua Tumaini kwa Haki ya Tabianchi”utaanza. Mkutano huo wa kimataifa unaandaliwa na Harakati ya Laudato Si' kwa kushirikiana na washirika mbalimbali wa kikanisa na kitaasisi, utaadhimisha kumbukumbu ya miaka kumi ya Waraka wa Baba Mtakatifu Francisko kuhusu utunzaji wa uumbaji.

Tukio hilo lililopangwa hadi tarehe 3 Oktoba 2025 kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari, litawaleta pamoja zaidi ya viongozi 400 wa kidini, wataalamu wa tabianchi, wawakilishi wa mashirika ya kiraia na taasisi mbalimbali duniani, kwa lengo la kupanga hatua zinazofuata katika kutekeleza uongofu wa kiikolojia kwa kuzingatia mafundisho ya Kanisa. Papa Leo XIV ataongoza "Sherehe ya Matumaini" Jumatano alasiri.

Kikao hicho kitakuwa na shuhuda mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Waziri wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi wa Brazili, Marina Silva, na Gavana wa zamani wa California Arnold Schwarzenegger, ambaye kwa muda mrefu amekuwa akijitolea kwa mipango kuhusu ulinzi wa viumbe. Baada ya hotuba ya Papa, kutakuwa na wakati wa ishara na  kiroho wa kujitolea kwa pamoja, ikifuatiwa na mkutano na kikundi cha washiriki wa mkutano. Siku zitakazofuata, Oktoba 2 na 3, zitakuwa na vipindi vya kufanya kazi, meza za pande zote, na nyakati za kiroho.

25 Septemba 2025, 17:37