Tafuta

Basilika ya Kuzaliwa kwa Yesu Basilika ya Kuzaliwa kwa Yesu  (©Custodia di Terra Santa)

Uratibu wa Nchi Takatifu:Gaza ni janga la kibinadamu!

Hija ya kila mwaka katika Nchi Takatifu inayofanywa na Maaskofu wa Ulaya na Amerika Kaskazini imehitimishwa,ikielezea ukaribu,mshikamano,na usaidizi wa kiroho na kichungaji kwa Jumuiya za Kikristo zinazoishi katika maeneo matakatifu."Jitihada za amani zishinde vurugu na kukomesha vitendo vya ugaidi na vita."

Vatican News

Katika taarifa ya mwisho iliyotolewa kwa vyombo vya habari iliyoandikwa na Maaskofu wa Ulaya na Amerika Kaskazini, wajumbe wa Uratibu wa Nchi Takatifu (HLC), walikuwa Hija katika Nchi Takatifu iliyohitimishwa hivi karibuni, kwa kuta maoni ya uchunguzi mchungu kwamba "Ilikuwa hija katika nchi ambayo watu wanapata kiwewe kikubwa."

Hii ni hija ya kila mwaka ya mshikamano, ambayo iliwapeleka, miongoni mwa matukio mengine, kwa Mabedouin wa Mihtawish wanaoishi Khan al-Ahmar (Mashariki mwa Yerusalemu) na katika kijiji cha Wakristo chaTaybeh katika Ukingo wa Magharibi, kilichoshambuliwa na walowezi wa Israeli.

2026.01.22 Pellegrinaggio

Wajumbe wa Hija ya mshikamano huko Nchi Takatifu.

Katikati ya Vurugu na Vitisho

Maaskofu walisikiliza historia, ushuhuda, na uzoefu wa maisha ya wale waliolazimishwa kuishi pembezoni, wakiwa na uhuru mdogo sana wa kutembea. "Tulisikia," taarifa hiyo inaendelea, "historia za mashambulizi ya walowezi wa Israeli na vurugu na vitisho vinavyoendelea, wizi wa mifugo, na ubomoaji wa mali, ambavyo huwaweka wengi macho usiku kwa kuhofia vurugu zaidi. Tulipowauliza ni nani aliyeona mapambano yao na kilio chao cha kuishi kwa amani na majirani zao, walijibu: 'Hakuna anayetuona.'"

Hali hiyo hiyo pia inatumika kwa jumuiya ya Wakristo huko Palestina, ambapo "walisimulia mateso yao: mashambulizi yasiyoisha ya walowezi wenye msimamo mkali, kung'olewa kwa miti ya mizeituni, kunyang'anywa ardhi, na vitendo vya vitisho vinavyofanya maisha yasivumilie, na kuwasukuma wengi kuhama kwa wingi." "Katika miezi kumi na miwili tangu ziara yetu ya mwisho," Maaskofu walisisitiza, "Nchi ya Ahadi imepunguzwa na kutiliwa shaka. Gaza bado ni janga kubwa la kibinadamu. Idadi ya watu wa Ukingo wa Magharibi tuliokutana nao wamevunjika moyo na wanaogopa. Sauti za ujasiri za Israeli zinazotetea haki za binadamu na za kiraia zinazidi kutishiwa; kuunga mkono sauti zilizotengwa ni kitendo cha gharama kubwa cha mshikamano. Tunaogopa kwamba wao pia watanyamazishwa hivi karibuni."

Kuhakikisha Haki za Wote

Katika kuthibitisha tena "haki ya Israeli ya kuwepo na ile ya Waisraeli kuishi kwa amani na usalama," maaskofu wa HLC wanaomba "kwamba haki hizi hizo zihakikishwe kwa wote waliojikita katika nchi hii." Kwa hivyo matumaini kwamba "juhudi za amani zitashinda vurugu na kwamba vitendo vya ugaidi na vita vitakoma." Kisha Maasofu wanazihimiza serikali kushinikiza Israeli kuheshimu utaratibu wa kimataifa unaotegemea sheria na kuanzisha tena mazungumzo yenye maana kuelekea suluhisho la mataifa mawili, kwa faida na usalama wa wote." Hija hiyo pia ilikuwa fursa ya kukutana na "ujasiri wa sauti za Wayahudi na Wapalestina ambao, licha ya matatizo makubwa na majeraha ya kibinafsi, wanaendelea kukuza haki, mazungumzo, na maridhiano."


Kutoa Sauti kwa Wasio na Sauti

"Kama Wakristo, ni wito na wajibu wetu kutoa sauti kwa wasio na sauti na kutoa ushuhuda wa utu wao, ili ulimwengu uweze kujua mateso yao na kusukumwa kukuza haki na huruma." Zaidi ya hayo, Maaskofu walisema wameguswa sana "na imani na uthabiti wa Wakristo wa eneo hilo na pia na watu wa imani zingine ambao wamejitolea kudumisha matumaini ya jamii zao. Mama au baba wanapotaka kukomeshwa kwa vurugu, dunia lazima isikilize na kutenda." Hatimaye, Uratibu wa Ardhi Takatifu unaitaka jumuiya ya kimataifa na wanaume na wanawake wote wenye mapenzi mema "kusimama pamoja na watu wa Nchi Takatifu.  Kutambua ombi lao la utu. Kusaidia kukuza mazungumzo ya kweli kati ya jamii. Kubali mwaliko wa Kardinali Pierbattista Pizzaballa, Patriaki wa Kilatini wa Yerusalemu, kwenda kuhiji kama ishara ya upendo wetu, msaada, na mshikamano."

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

22 Januari 2026, 14:20