Tafuta

Maendo ya Nchi Takatifu Maendo ya Nchi Takatifu 

Yerusalemu,Hija ya 2026 Uratibu wa Nchi Takatifu

Maaskofu wa Baraza la Maaskofu wa Uswiss,Ujerumani,Uingereza na Galles,Canada,Denmark,Scotland,Hispania,Marekani,Finland,Ufaransa,Ireland,Iceland,Italia,Norway na Sweden,wako Nchi Takatifu kuanzia tarehe 17 hadi 22 Januari 2026 ili kuonesha mshikamano kwa Jumuiya za Kikristo mahalia na kisha kutoa taarifa kwa nchi zao husika.

Vatican News

Tangu tarehe 17 hadi 22 Januari 2026 inaendelea hija ya kuitamaduni ya kuwa  huko Yerusalemu ya Uratibu wa Nchi Takatifu, ikishirikisha Maaskouf wanaowakilisha Mabaraza ya maaskofu ya Uswiss, Ujerumani, Uingereza na Wales, Canada, Denmark, Scotland, Hispania, Marekani, Finland, Ufaransa, Ireland, Iceland, Italia, Norway na Sweden. Askofu Nicolò Anselmi wa Rimini anashiriki kama mwakilishi wa Baraza la  Maaskofu  nchini Italia (CEI).

Ratiba

Ratiba yao pamoja na mengine ya Maaskofu kwa siku za hija ni kukutana na Patriaki wa Kilatini wa Yerusalemu, Kardinali Pierbattista Pizzaballa, Balozi wa Vatican nchini Israeli, Mjumbe wa Kitume nchini Yerusalemu na Palestina, Askofu Mkuu Adolfo Tito Yllane, na Paroko wa Parokia ya  Gaza, Padre Gabriel Romanelli, wakati wa mkutano wa mtandaoni.

Ratiba nyingine ilikuwa ni kukutana na Masista wa Comboni, ambao wamekuwa wakishirikiana na jumuiya za Wabedouin kwa muda mrefu, ambapo waliadhimisha Misa ya Dominika tarehe 18 Januari 2026 na Wakatoliki wa Taybeh, walishiriki siku hiyo na jumuiya za Wakatoliki wa Kigiriki wa Melkite na Waorthodox wa Kigiriki.

Kujitolea kwa Kanisa kwa Jumuiya mahalia

Mabadilishano ya maoni mbalimbali ya pamoja na Vikariate ya Mtakatifu James, Kituo cha Rossing cha Elimu na Mazungumzo, na Wakuu wa Kiyahudi wa Haki za Binadamu, kuonesha kujitolea kwa Kanisa Katoliki kwa mazungumzo na utu wa binadamu katika muktadha tata yalipangwa. Zaidi ya hayo, ziara ya kichungaji katika Seminari ya Mapatriaki wa Kilatini huko Bethlehemu ilipangwa, kwa mada "Nchi ya Ahadi: Kukutana na Mazungumzo na Watu Wanaoleta Matumaini."

Seminari hiyo inawafunza Mapadre wa baadaye na watu wa kawaida waliojitolea kutumikia Kanisa mahalia katika mazingira yenye sifa ya udhaifu. Mkutano huu ni sehemu ya hija inayoendelea ya mshikamano, ikithibitisha kwamba Kanisa katika Nchi Takatifu haliko peke yake na kwamba Nchi ya Ahadi inabaki kuwa mahali ambapo matumaini hujengwa na kushirikishwa.

Ziara, Mikutano, na Nyakati za Maombi

Uratibu wa Nchi Takatifu kwa kawaidia hukutana kila mwaka ili kuonesha ukaribu, mshikamano, na msaada wa kiroho na kichungaji kwa jumuiya za Kikristo zinazoishi katika maeneo ambayo Yesu aliishi. Kupitia ziara, mikutano, na nyakati za maombi, Maaskofu walikusudia kuwakumbusha Wakristo wa eneo hilo kwamba hawako peke yao, kuhimiza hija, na kuweka umakini wa Kanisa zima ukizingatia changamoto zinazokabili Nchi Takatifu.

Uratibu wa Nchi Takatifu ni kundi la kimataifa la Maaskofu ambao, kwa niaba ya Mabaraza yao  ya Maaskofu, husafiri kwenda Nchi Takatifu kila mwaka kuonesha mshikamano na jumuiya za Wakristo wa eneo hilo na kisha kutoa ripoti kwa nchi zao husika. Kila mwaka, wanaambatana na mapadre na watu wataalamu wa kawaida. Kanisa la Italia limeonesha ukaribu mkubwa na Nchi Takatifu kupitia udugu wa Kanisa, Mipango inayoungwa mkono na kodi ya walipa kodi ya 8Xmille, na mipango inayoendelezwa na majimbo na parokia zote nchini Italia.

"Nitarudisha Rimini, kwa jimbo letu, na kwa Kanisa la Italia sauti, uzoefu, na sala zilizosikika wakati huo," alisema Askofu Mkuu Anselmi, ambaye ataandaa ripoti kwa  ajili ya Mkutano Mkuu wa Mkutano wa Baraza la Maaskofu wa Italia.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

 

20 Januari 2026, 14:45