Tafuta

Siku ya Lugha ya Kiswahili Duniani 2026:Kiswahili kwa ajili ya amani,mshikamano na diplomasia ya uchumi duniani" Siku ya Lugha ya Kiswahili Duniani 2026:Kiswahili kwa ajili ya amani,mshikamano na diplomasia ya uchumi duniani"  (Tanzania State House)

Siku ya Lugha ya Kiswahili Duniani 2026:ujenzi wa amani,maendeleo endelevu&diplomasia ya kiuchumi

Siku ya Lugha ya Kiswahili Duniani,iliyotangazwa na Mkutano Mkuu wa UNESCO mwaka 2021,inatambua umuhimu wa Kiswahili kama mojawapo ya lugha zinazozungumzwa sana duniani na kama chombo chenye nguvu cha mazungumzo ya kiutamaduni.Ni katika muktadha huo UNESCO imeandaa Julai 6 na 7 katika Makao makuu yake toleo la II la 2026 Kimataifa ili kusisitiza zaidi mchango wa lugha hiyo"katika ujenzi wa amani,maendeleo endelevu na diplomasia ya kiuchumi."

Na Angella Rwezaula 

Tunapofikiria lugha, tunafikiria chombo kinachotumiwa na watu kujiwakilisha, kwa hivyo tujue zaidi kwamba nyuma yake kuna utamaduni unaounga mkono chombo hicho. Pia inawezekana kuthibitisha kuwa utamaduni haupo, au haupaswi kujadiliwa, bila kuzingatia chombo cha lugha. Utamaduni unaelezewa au kufafanuliwa kupitia lugha hiyo. Lugha kwa kawaida inakua kwa sababu ya uhamiaji kama shinikizo na fursa ya mabadiliko makubwa ya utamaduni. Kujifunza lugha ni mbio ndefu, japokuwa siyo kasi. Ili kuendelea katika safari hiyo, mazoezi ya mara kwa mara na ya kudumu ni muhimu. Lugha inaunganisha, inatambulisha inaendelezwa na ikitumiwa vizuri inakuwa fursa ya kufungamanisha na kuleta maendeleo na amani. 

UNESCIO:Siku ya Lugha ya Kiswahili duniani 2026

Katika muktadha wa lugha za kimataifa, kuanzia tarehe 6 hadi 7 Julai 2026 katika Makao Makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, utamaduni, sayansi na Teknolojia (UNESCO),jijini Paris, nchini Ufarasa  litafanyika toleo la Siku ya Lugha ya Kiswahili Duniani 2026(Kiswahili World Language Day 2026). "Toleo hili  litaleta pamoja wahusika wakuu katika kuhamasisha na kusambaza Kiswahili, kuanzia wadau wa ngazi ya juu hadi wawakilishi wa kijamii. Kupitia mikutano, maonesho na mabadilishano ya ngazi ya juu, maadhimisho hayo yataakisi jukumu la Kiswahili kama lugha ya amani, mazungumzo, utambulisho wa kiutamaduni, elimu, ujumuishaji wa kikanda na ushirikiano wa kimataifa," Kwa mujibu wa waandaaji

Katika toleo hii kwa mujibu wa taarifa, "Utafsiri mbashara kwa Kiswahili utapatikana katika vipindi vyote vya programu." Hata hivyo wanabainisha kwamba, "Siku ya Lugha ya Kiswahili Duniani, iliyotangazwa na Mkutano Mkuu wa UNESCO mwaka 2021, inatambua umuhimu wa Kiswahili kama mojawapo ya lugha zinazozungumzwa sana duniani na kama chombo chenye nguvu cha mazungumzo ya kiutamaduni." Kwa njia hiyo " Toleo la 2026 litasisitiza zaidi mchango wa lugha hiyo katika ujenzi wa amani, maendeleo endelevu na diplomasia ya kiuchumi, hasa katika muktadha wa ujumuishaji wa kikanda wa Afrika na ushawishi unaoongezeka duniani."

Ratiba kwa ujumla

Ni "Mkutano wa Pili wa Kimataifa kuhusu Lugha ya Kiswahili. Maonesho yataendelea, yakitoa nafasi ya mitandao, kubadilishana maarifa na ushiriki wa umma kuhusu maendeleo ya Kiswahili. Hafla rasmi itawakutanisha wawakilishi wa ngazi ya juu, Mabalozi na Wajumbe wa Kudumu wa UNESCO, wajumbe wa kikosi cha kidiplomasia, Sekretarieti ya UNESCO, asasi za kiraia, wasomi, sekta binafsi na jamii za diaspora," ratiba inaonesha.

Kwa njia hiyo hata hotuba na maonesho mbali mbali:  "Hafla hiyo itajumuisha hotuba za wawakilishi wa Kundi la Afrika, UNESCO na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na maonesho ya kiutamaduni, onesho la mitindo ya Kiswahili, hotuba za Mgeni Rasmi, uwasilishaji wa tuzo zinazotambua michango katika kukuza Kiswahili, na picha ya pamoja. Washiriki wataalikwa kugundua mila na tamaduni  za mapishi ya Kiswahili  ya  Afrika Mashariki katika Uwanja wa Makao Makuu ya UNESCO, yakiambatana na maonesho ya kiutamaduni."

Unaweza kujiandikisha kwa kubonyeza linki ifuatayo: https://indico.un.org/event/1024664/registrations/27098/

Kwa  kujua mengine zaidi tembelea tovuto: https://www.unesco.org/en/articles/world-kiswahili-language-day-2026-kiswahili-peace-solidarity-and-global-economic-diplomacy

UNESCO: SIKU YA KISWAHILI JULAI 6 NA 7.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku.  Just click here.

30 Juni 2026, 13:53